Waziri Mkuu wa Tanzania, Mh. Mizengo Pinda |
Dar es Salaam, Jumatatu
Februari 16 2015 – Taasisi
ya Uongozi wa Afrika kwa Maendeleo Endelevu (UONGOZI Institute) imeandaa mkutano
wa kikanda utakaokutanisha
viongozi na watunga sera kutoka nchi za
Afrika mashariki kuzungumzia changamoto za ukuaji wa miji na kushughulikia hali
ya baadaye ya miji ya Afrika.
Mkutano huu uliopewa jina la, ‘Maisha ya baadae ya
nchi za Afrika Mashariki: Jinsi gani tunataka kuishi mwaka 2050’, utafanyika
katika hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, Kilimanjaro Hotel tarehe 19 na
20 Februari ambapo Waziri Mkuu wa Tanzania, Mh. Mizengo Pinda (Mb), atakuwa
mgeni rasmi.
“Kuna uwiano mkubwa wa ongezeko la watu Afrika (na
duniani kwa ujumla) wanaoishi mijini na kupelekea msongamano na shinikizo la
nyumba, ajira na huduma za kijamii. Ni kwa matokeo haya jukwaa hili limelenga
kujadili namna ya kutatua changamoto hizo na kufikiria miji ambayo itatimiza
matakwa yetu,” alisema Prof. Semboja.
Kwa mujibu wa chapisho la UN-Habitat ‘Hali ya miji ya Afrika 2014’ , “Afrika
Mashariki inashika nafasi ya chini katika miji inayokua duniani lakini ndiyo
kanda inayoongoza katika kasi ya ukuaji wa miji yake hivi sasa. Ifikapo mwishoni mwa muongo huu wa sasa idadi
ya wakazi waishio mijini itaongezeka kwa asilimia 50 na jumla ya idadi ya
wakazi wa mijini ifikapo mwaka 2040 inatarajiwa kuwa mara tano ya 2010.
Hivyo basi, ukanda wa Afrika Mashariki utakumbwa na
changamoto zitakazotokana na ongezeko kubwa la
idadi ya watu mijini; ongezeko kubwa la madai mapya na ya ziada kwa
ajili ya utoaji wa nyumba za kutosha na kwa gharama nafuu na huduma mijini, na
pengine muhimu zaidi, fursa ya kuzalisha kipato mijini.”
“Ni dhahiri kwamba ukuaji wa miji na maendeleo mijini
ni matokeo chanya ya maendeleo ya binadamu na ukuaji wa kiuchumi kama tunaweza kuyakabili
kiusahihi. Na hii ndiyo maana nzima ya mkutano huu…Kutuweka katika njia sahihi
kwa kutambua vipaumbele vya juu na vitu muhimu kwa ajili ya maendeleo," aliongeza
Prof. Semboja.
Washiriki wa kongamano hili watatoka: Burundi,
Ethiopia, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudan ya Kusini, Tanzania na Uganda. Waalikwa watakuwa wawakilishi wa ngazi
za juu kutoka serikalini, mashirika ya kikanda na kimataifa, miji mikubwa,
wasomi, sekta binafsi na asasi za kiraia.
Kwa maelezo zaidi
wasiliana na:
Mr. Amani Nkurlu, Afisa Mawasiliano , UONGOZI Institute
Simu: +255 22 2602917, +255 0712 223 839
Barua pepe: ankurlu@uongozi.or.tz
www.uongozi.or.tz
No comments:
Post a Comment