Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 11 February 2015

MKAZI WA MWANZA ASHINDA BAJAJI YA SITA YA PROMOSHENI YA 'TUTOKE NA SERENGETI'

Meneja Chapa wa bia ya Serengeti premium lager, Rugambo Rodney, (kulia) akiongea kwa njia ya simu na mshindi wa sita wa Limo Bajaji, Ramadhani Abubakar, katika shindano la 'Tutoke na Serengeti' lililofanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni msimamizi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha, Baraka Majid.
Meneja Chapa wa bia ya Serengeti premium lager, Rugambo Rodney, (katikati) akiongea kwa njia ya simu na mshindi wa sita wa Limo Bajaji, Ramadhani Abubakar, katika shindano la 'Tutoke na Serengeti' lililofanyika jana makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni msimamizi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha, Bw. Baraka Majid na kulia ni msimamizi kutoka PriceWaterhouseCoopers, Golder Kamuzora.
Meneja Chapa wa bia ya Serengeti premium lager, Rugambo Rodney, (katikati) akibonyeza kitufe wakati wa kutafuta mshindi wa sita wa Limo Bajaji, katika shindano la 'Tutoke na Serengeti' lililofanyika makao makuu ya kampuni hiyo Chang'ombe jijini Dar es Salaam. Kushoto ni msimamizi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha, Baraka Majid na kulia ni msimamizi kutoka PriceWaterhouseCoopers, Golder Kamuzora.
Bajaji ya sita ya kampeni ya Tutoke na Serengeti, safari hii itaelekea mkoani Mwanza baada ya bwana Ramadhan Abubakar kutangazwa kuwa mshindi wa Limo Bajaji, kufuatia ushiriki wake yakinifu tangu kuanza kwa kampeni hii.

Akiongea kwa njia ya simu, Abubakar (28) ambaye ni fundi umeme na mkazi wa Nyamagana, Mwanza alielezea furaha yake baada ya kuelezwa na SBL kwamba ameshinda Limo Bajaji mpya katika kampeni ya Tutoke na Serengeti…. “Aisee Mungu ni Mwema,…alitahamaki,… asante sana kwa kunipa habari hii njema sikutarajia kushinda kabisa.”


Baada kuulizwa ni kwa namna gani ataitumia bajaji aliyoshinda katika shughuli zake za kila siku, alisema ataitumia Bajaji hii kwa shughuli za usafirishaji. Mwakazi aliongeza kwamba bajaji hiyo itamsaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza kipato cha familia kwa zaidi ya asilimia 50 huku akiwa na lengo la kujiendeleza kitaaluma kwenye ufundi umeme.

Akiongea na vyombo ya habari leo katika makao makuu ya SBL yaliyoko Chang’ombe Dar es salaam, Meneja Chapa wa bia ya Serengeti Premium Lager Mr. Rugambo Rodney alisema, “Mshindi wetu wa sita wa Limo Bajaji nae anatoka nje ya Dar es salaam kuashiria kwamba kampeni hii imepokelewa vizuri mikoani kinyume na ilivyozoeleka na watu wengi kwamba kampeni za namna hii ni za wakazi wa Dar es Salaam tu. Rodney aliongeza kuwa kwa sasa imebaki nafasi moja ambayo ni ya Mtoko wa mbugani huku akiwahimiza wateja kutumia mwezi huu wa wapendanao kuwa “Surprise” na kutoa zawadi ya “Mtoko wa mbugani" kwa wenza wao ndani ya hifadhi ya taifa ya Serengeti.

Kwa upande mwingine ujumbe kutoka B-PESA wataalam wa teknolojia ambao katika promosheni hii wanahusika na usambazaji wa fedha kwa washindi kupitia njia ya simu maeneo mbalimbali hapa nchini, imethibitisha kuwalipa fedha taslim washindi wa kila wiki.

Ili kushiriki katika promosheni hii, mteja anatakiwa awe na umri wa miaka 18, anunue Serengeti Premium Lager na aangalie chini ya kizibo ambapo atakutana na namba maalum anazotakiwa kuzituma kwa njia ya sms kwenda 15317. Kadiri unavyoshiriki mara nyingi ndivyo unavyojiweka katika nafasi ya ushindi.

No comments:

Post a Comment