Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday, 20 February 2015

BENKI YA STANDARD CHARTERED YAZINDUA “KOMBE LA STANDARD CHARTERED TROPHY – NJIA KWENDA ANFIELD 2015”

Mkuu wa kitengo cha Wateja wa Makampuni Makubwa wa Benki ya Standard Chartered, Femi Alonge, akipiga mpira kuashiria uzinduzi wa shindano la soka la “Kombe la Standard Chartered – Njia Kwenda Anfield” katika ofisi za Benki hiyo. Wakishuhudia tukio hilo ni: kutoka kulia kwenda kushoto: Ruth Zaipuna – Mkuu wa Kitengo cha Fedha, Michael Shio – Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na Juanita Mramba – Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Masoko.
Tanzania, Alhamisi 19, 2015: Benki ya Standard Chartered Bank Tanzania imezindua shindano kabambe la mpira wa miguu liitwalo “Kombe la Standard Chartered – Njia Kwenda Anfield”. Shindano hili la kimataifa ambalo litahusisha wachezaji watano katika kila timu, limeandaliwa na Benki ya Standard Chartered ikishirikiana na klabu ya Liverpool, kuwapa wapenzi wa mpira nafasi ya kihistoria na ya kipekee kuweza kucheza kwenye viwanja vya klabu ya Liverpool huko Anfield.

Wakati Benki ya Standard Chartered ikizindua shindano hili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania, shindano hili limekuwa likifanyika katika Benki hiyo katika nchi mbalimbali kwa miaka kadhaa tangu Benki hiyo ilipoanza kudhamini klabu ya Liverpool hapo mwaka 2010. Mei Mwaka jana, udhamini huo wa Benki ya Standard Chartered kwa klabu ya Liverpool ulipata tuzo ya shirika la michezo la BT – Best International Marketing Campaign - ikiwa ni tuzo kubwa zaidi katika sekta ya michezo na masoko.

Shindano hili litakuwa na hatua tatu; mechi za kufuzu kitaifa, ambazo zitachezwa katika nchi mbalimbali zitakazoshiriki kwenye shindano hili ikiwa ni pamoja na Kenya, Uganda na Tanzania zikiwasilisha Afrika Mashariki, Botswana, Zambia na Zimbabwe zikiwakilisha Afrika Kusini na Gambia, Ghana na Nigeria zikiwasilisha Afrika Magharibi. Nchi nyingine zitakazoshiriki ni India na Sri Lanka zikiwakilisha Asia Kusini, Vitenam, Singapore na Malaysia zikiwakilisha Asia Kusini Mashariki, na nchi nyinginezo. Hatua ya pili itakuwa mechi ya kufuzu kikanda ambapo timu ya itakayofuzu Tanzania itakwenda kupamba na timu za Kenya na Uganda. Hatua ya tatu nay a mwisho itakuwa mechi la kuwania kombe hilo zitakazofanyika katika viwanja vya Anfield nchini Uingereza.

Mechi za kufuzu shindano la kitaifa zitafanyika tarehe 28 Februari, 2015, ambapo jumla ya timu timu 32, zikiwa ni makampuni mbalimbali wateja wa Benki hiyo, timu za waandishi wa habari na wadau wengine wa benki hiyo watapambana katika kinyang’anyiro cha kumtafuta mshindi wa Tanzania katika viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam.

Baada ya hapo mashindano ya kanda ya Afrika Mashariki yatafanyika Nairobi, Kenya, tarehe 7 Machi, 2015 na washindi wa kanda ya Afrika Mashariki watakwenda nchini Uiengereza na kupambana na timu nyingine kumi kutoka Afrika Magharibi, na Afrika Kusini na timu nyingine kutoka mabara mengine kuwania Kombe hilo la Standard Chartered. Mechi za fainali zitafanyika tarehe 7 na 8 Mei, 2015.

Akitangaza zawadi za shindano hilo, Mkuregenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Liz Lloyd, alisema, “Zawadi ya shindano hili itakuwa ni ile nafasi ya kipekee ya kuweza kucheza kwenye himaya ya klabu ya Liverpool, Anfield, kule Uiengereza. Zaidi ya Benki yetu kulipia safari na gharama zote za safari za Nairobi na Uiengereza, timu zitakazoshinda zitakuwa na siku tatu nzima nchini Uiengereza ambapo watapata fursa ya kukutana na kufunzwa soka na manguli wa mchezo huu wa timu ya Liverpool, kama vile John Barnes na wengineo”.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa mialiko tayari imeshatumwa kwa makampuni mbali mbali ambayo ni wateja wa Benki hiyo, waandidhi wa habari na wadau wengine wa Benki hiyo na kuwa washiriki watachaguliwa kwa jinsi ambavyo watajisali haraka kufuatia mialiko hiyo ambapo usajili utafungwa tarehe 23 Februari, 2015.

“Tunataka kuwapa wateja wetu, wafanyakazi wetu na waandishi wa habari nafasi hii ya kipekee na ningependa kuongeza kuwa itabidi timu yetu ya Tanzania icheze kwa biddi pale Nairobi ili kuzishinda timu za Kenya and Uganda na kuweza kwenda Uiengereza. Ningependa kweli timu ya Tanzania ishinde Kombe hili pale Anfield, Uingereza.” Liz aliongeza.

Kwa upande wake, Charles Katongole, ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Soko la Fedha, ambaye pia anaratibu mradi huo kwa upande wa Uongozi wa Benki hiyo alisema, “Watanzania tunapenda mpira, haswa wa Ligi ya Uingereza. Sisi kama Benki ya Standard Chartered tunafurahia ushirikiano wetu na klabu ya Liverpool na tunataka kuwapa wateja wetu na wadau wetu wa karibu fursa ya kuweza kuufurahia ushirikiano huu kwa kupitia shindano hili. Ninaamini kuwa tutakuwa na mashindano mazuri katika hatua zote tatu na tunawakaribisha wadau wetu wajitokeze kwa wingi”

For further information please contact:

Beda M. Biswalo
Corporate Affairs Manager
Standard Chartered Bank Tanzania
Tel: +255222164920
Mobile: +255788455234
Email: BedaMichael.Biswalo@sc.com

Juanita Mramba
Head of Corporate Affairs, Brand & Marketing
Standard Chartered Bank Tanzania
Tel: +255222164920
Mobile: +255767393992
Email: Juanita.Mramba@sc.com

No comments:

Post a Comment