Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma (PAC), Mh. Zitto Kabwe (wa tatu kulia) akizungumza wakati akiongoza kikao cha Kamati yake na Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kilichofanyika kwenye ofisi ndogo za Bunge, Jijini Dar es salaam leo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade akizungumza katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma (PAC) na Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kilichofanyika kwenye ofisi ndogo za Bunge, Jijini Dar es salaam leo.
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma (PAC), imeitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kufanya uchunguzi wa sukari kutoka nje inayoingizwa nchini kwa njia ya panya, kwani inaua viwanda vya sukari vilivyopo nchini.
Akizungumza na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Zitto Kabwe amesema TRA inatakiwa kufanya kazi katika kudhibiti mianya inayoisababishia mamlaka kukosa mapato. Amesema katika agizo la kamati wameiagiza TRA katika ripoti za forodha kuweka misamaha ya kodi ili kuweza kujua ni misamaha mingapi inaingizwa katika ushuru wa forodha.
Kamati hiyo iliipongeza TRA kwa kurasimisha kazi za wasanii ambayo imeweza kuliingizia Taifa Sh. milioni 348 kwa mwaka jana hivyo wanawajibu wa kuendeleza ili kuweza kuondoa wizi wa kazi zao pamoja na kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) ili wananchi waweze kupata tiketi kwa mfumo wa eletroniki kwa kuweza kuweka zawadi za kuwavutia na huduma hiyo.
Hata hivyo kamati imeiagiza wizara ya fedha ianze kutekeleza sheria mpya ya ongezeko la thamani (VAT) na TRA inawajibu wa kufatilia agizo hilo kwa waziri na kanuni zake za sheria hiyo inatakiwa kuwa tayari.
Zitto amesema makusanyo ya TRA yaendane na bajeti na ni lazima wakusanye zaidi ili kuweza kuweka malengo yao ikiwa ni pamoja na kushughulikia changamoto na kuweza kufikia malengo ya 2025.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

No comments:
Post a Comment