Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 15 October 2014

WATEJA WATATU WA NBC WAIBUKA KIDEDEA KATIKA PROMOSHENI YA WEKA UPEWE

Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC, Rukia Mtingwa (kulia) akifanya mahojiano na waandishi wa habari wakati wa droo ya kwanza ya promosheni ya Weka Upewe jijini Dar es Salaam leo.

Mkazi wa Jiji la Dar es Salaam, Job Mwakibinga (kulia) akibonyeza kompyuta ili kupata washindi watatu wa droo ya kwanza ya promosheni ya Weka Upewe ya benki ya NBC jijini Dar es Salaam leo. Wanaoangalia kutoka kushoto ni Meneja Mahusiano wa benki hiyo, Subira Mwaya, Meneja katika Kitengo cha Kuwekeza na Wateja Wakubwa, Dorothea Mutatembwa na Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Mrisho Millao. Dk. Nyagosya Range wa Dar es Salaam alishinda bajaji, Stella Kivuyo na Mchungaji Christopher Kingo wa Karatu, Arusha walijishindia pikipiki.

Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, Subira Mwaya (kushoto) akizungumza kwa simu na mmoja wa washindi wa droo ya kwanza ya promosheni ya Weka Upewe jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni Meneja katika Kitengo cha Kuwekeza na Wateja Wakubwa, Dorothea Mutatembwa, Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Mrisho Millao na mfanyakazi wa benki hiyo Tawi la Mlimani,Elizabeth Kinyonto.

Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC, Rukia Mtingwa (katikati) akizungumza wakati wa droo ya kwanza ya promosheni ya Weka Upewe jijini Dar es Salaam leo. Wengine kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa, Andrew Massawe na Meneja katika kitengo hicho, Dorothea Mutatembwa. (Picha na Peter Mgongo)

No comments:

Post a Comment