Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 14 October 2014

MAJUMUISHO YA MAJADILIANO YA AWALI KATI YA TANZANIA, BENKI YA DUNIA NA IMF

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dr. Servacius Likwelile ambaye ni kiongozi wa ujumbe kutoka Tanzania na anawakilisha kama Gavana Mbadala (Alternate Governor) pamoja na Gavana wa Benki Kuu, Prof. Benno Ndulu ambaye pia ni Gavana katika mikutano hii. Katika picha viongozi hao wakiwa wanafanya majumuisho ya majadiliano ya awali na kukubaliana cha kufanya kwa pamoja na viongozi kutoka IMF na WB kuhusiana na hali ya uchumi kwa maana ya sera za fedha na sera za mapato na matumizi.

Bw. Herve’ Joly ambaye ni Mkurugenzi msaidizi na Mkuu wa idara ya Afrika sehemu ya Mashariki akimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali, Dr. Servacius Likwelile (hayupo katika picha), alipokuwa akitoa msimamo wake kuhusu sera zinazopendekewa na IMF na WB.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile alipokuwa akitoa msimamo wake kuhusu sera zinazopendekewa na IMF na WB.

Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali akiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania wakichukua mapendekezo kutoka kwa viongozi wa IMF na WB (hawapo kwenye picha). Kutoka kushoto ni Gavana wa Benki kuu ya Tanzania akiwa amefuatana na Bi. Natujwa Mwamba Naibu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania na kutoka kulia ni Bw. Philip Mpango Katibu Mtendaji tume ya Mipango akifuatiwa na Msaidizi wa kamishna sera Bw. Shogholo Msangi na wa mwisho ni Kamishna wa Bajeti Bw. John Cheyo na walioketi nyuma wote ni wajumbe kutoka Tanzania.

Michuzi Blog

No comments:

Post a Comment