Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday 6 October 2014

CHARLES KIMEI AJUMUIKA NA WAFANYAKAZI WA CRDB, KIJITONYAMA KATIKA KUWAHUDUMIA WATEJA WA BENKI HIYO IKIWA NI SEHEMU YA MAADHIMISHO YA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akitoa ufafanuzi kwa mteja wa Benki ya CRDB kuhusu huduma mbalimbali za benki hiyo. Dk. Kimei alijumuika na wafanyakazi wa tawi la Kijitonyama katika kuwahudumia wateja wa benki hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya wateja wa Benki hiyo inayoanza Oktoba 6.

Baadhi yawateja wakimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei baada ya kupata huduma katika tawi la Kijitonyama.

Baadhi ya wateja wakimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei baada ya kupata huduma katika tawi la Kijitonyama.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akigonga muhuri katika cheki ya mteja.

Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akiwa na Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Silvia Lupembe.

Dk. Kimei akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa wateja waliofika katika tawi la Benki ya CRDB Kijitonyama kupata huduma.

Dk. Kimei akimsikiliza mteja wa Benki ya CRDB tawi la Kijitonyama.

Wateja wakipata huduma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kushoto) akijaza fomu ya kufungua akaunti ya Junior Jumbo  kwa ajili ya mtoto Daud Stephen (6) (katikati) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Wateja wa Benki iliyoanza jijini Dar es Salaam.

Keki iliyopambwa vizuri ikisubiri kukatwa kwa ajili ya wateja na wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Kijitonyama ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wateja wa Benki ya CRDB.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akikata keki ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wateja wa Benki ya CRDB.

Mteja mdogo kuliko wote wa tawi la Kijitonyama, Daud Mwakwenda (6) akilishwa keki na Dk. Kimei wakati wa hafla hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Maxcom, Juma Rajabu akilishwa keki na Dk. Kimei.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akimkabidhi maua mteja wa Benki ya CRDB aliyefika katika tawi la Kijitonyama.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akiwa katika picha ya pamoja na wateja wa Benki ya CRDB na maofisa wa benki hiyo.

No comments:

Post a Comment