Pichani ni Meneja wa Tawi lililopo ndani ya maonyesho ya biashara ya Kimataifa ya 38 yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwl .Julius Nyerere jijini Dar, Bi. Upendo Tendewa akifafanua zaidi huduma zitolewazo na benki hiyo. Bi. Upendo amesema kuwa dhamira yao kubwa ni kukidhi mahitaji ya wateja ya kibenki na ya kifedha kwa kuhakikisha upatikanaji wa bidha na huduma bora kabisa katika soko kwa bei inayowezekana kulipa na viwango vyenye manufaa yanayolingana na gharama na faida ya kurudhisha kwa mwanahisa.
Amesma benki hiyo inatumia kadi yako iitwayo Twiga ExpressCard ambayo mteja anaweza kuitumia kupata huduma za kibenki katika ATM yoyote iliyounganishwa na mtandano wa UMOJA SWITCH, ambapo zaidi ya ATM 180 na mabenki ishirini nna nne nchini yameunganishwa. Afisa Masoko wa Benki ya Twiga Bancorp Bw. Adalbert Alchard akizungumza na Wanahabari nje ya banda lao kuhusiana na huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo kwa wateja wao, kwenye maonyesho ya biashara ya Kimataifa ya 38 yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwl. Julius Nyerere jijini Dar. Pichani kushoto ni Afisa wa Benki hiyo, Bi Tuddy Lutengan - moblog
No comments:
Post a Comment