Wadau wakiendelea kumiminika kwa wingi kwenye banda la Benki Kuu lililopo kwenye Viwanja vya Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa, Jijini Dar es Salaam (Saba Saba).
Mmoja wa Maafisa wa Benki Kuu akitoa maelezo kwa Wadau waliotembelea kwenye banda hilo ili kufahamu maswala mbali mbali ya Kibenki, wakati wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Saba Saba, Jijini Dar es Salaam.
Maafisa wa Benki Kuu wakiendelea kutoa somo kwa watu mbali mbali waliofika kwenye banda hilo, huku moja ya somo ni lile la kuweza kutambua na kutofautisha noti bandia na noti halali.
Benki Kuu yatoa sarafu ya jero (mia tano) kama ionekanavyo pichani , ila bado haijaingia mtaani mpaka hapo itakapotangazwa rasmi kuanza kwa matumizi yake.
Kwa picha zaidi, bofya hapa.
No comments:
Post a Comment