Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Amanzi (kushoto) akipokea kitabu chenye mafundisho ya kifedha yanayofuata maadili ya kiiislamu kutoka kwa Meneja Tawi wa Benki ya NBC Morogoro, James Ndimbo wakati wa semina iliyoandaliwa kwa wateja wanaotumia huduma za kibenki zinafuata misingi ya kiislamu (NBC Islamic Banking ), iliyofanyika mjini humo hivi karibuni. Anayeangalia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoa wa Morogoro, Bachoo S. Bachoo.
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Industrial, Judith Motta, (kulia) akiwafundisha kusoma baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Child in the Sun ikiwa ni sehemu ya mpango wa mameneja wa benki hiyo kanda ya Dar es Salaam hivi karibuni kujitolea muda wao kufundisha kwenye vituo mbalimbali vya watoto wanaoishi katika vituo vya watoto wenye mahitaji. Wanafunzi wapatao 27 katika kituo hiki kinachokusanya watoto toka mitaani na kuwalea chini ya uangalizi wenye maadili mzuri na mafunzo ya kazi za mikono hawajui kusoma wala kuandika.
Baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Child in the Sun kilichopo Mbezi Makabe wakifanya mazoezi ya kusoma na kuandika baada ya kutoka madarasani walikkofundishwa na timu ya Mameneja wa matawi ya NBC yaliyoko Kanda ya Dar Salaam. Tathmini ya wiki ya tatu inaonyesha watoto wote wameshajua kusoma na kuandika na changamoto inayofuata ni kuunganisha maneno na kutunga tungo zenye kuleta maana.
No comments:
Post a Comment