Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Monday, 8 December 2025

BENKI YA STANBIC YACHANGIA MADAWATI KWA SHULE YA IHOMBWE, MKOANI MBEYA

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Brigedia Jenerali Maulid Sulumbu (kushoto), ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mh. Beno Malisa, akimkabidhi miche ya miti, meza na viti Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbeya, CPA Ndinda Njile, baada ya kupokea msaada wa vifaa hivyo kutoka kwa Meneja wa Benki ya Stanbic Tawi la Mbeya, Paul Mwambashi (nyuma, kushoto). Vifaa hivyo, vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20, vimetolewa na benki hiyo kwa ajili ya Shule ya Sekondari Ihombwe iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.

Benki ya Stanbic Tanzania imeendelea kuonyesha dhamira yake ya kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha miundombinu ya elimu nchini, baada ya kukabidhi jumla ya meza 120, viti 120 na miche ya miti 100 kwa Shule ya Sekondari Ihombwe iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Vijijini, Kata ya Utengule Usangu. Vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 vilikabidhiwa Desemba 4, 2025.

Wito wa Kulinda Amani na Mshikamano

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mh. Beno Malisa, kupitia mwakilishi wake Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Jenerali Majid Hassan Sulumbu, alitoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Mbeya kulinda tunu za taifa—amani, umoja na mshikamano—hasa tunapoelekea kwenye sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya 2026.

Amesema kuwa jitihada za wadau kama Stanbic zinachangia sio tu katika maendeleo ya sekta ya elimu, bali pia katika kujenga taifa lenye umoja na ustawi wa kijamii.

Stanbic Yapongezwa kwa Kujitoa Kwao

Mh. Jenerali Sulumbu ameipongeza Benki ya Stanbic kwa mchango wao muhimu katika kuendeleza miundombinu ya elimu, akisisitiza kuwa ni mfano unaopaswa kuigwa na wadau wengine.

Ameongeza kuwa serikali ya awamu ya sita itaendelea kushirikiana na sekta binafsi kuhakikisha mazingira ya kujifunzia yanaimarishwa katika maeneo yote nchini.

Stanbic Yaendelea Kutoa Huduma Bora kwa Miaka 30

Kwa upande wake, Meneja wa Benki ya Stanbic Tawi la Mbeya, Paul Mwambashi, ameitaka jamii kuendelea kutumia huduma mbalimbali kupitia benki hiyo, akibainisha kuwa kwa miaka 30 ya kutoa huduma za kifedha nchini, Stanbic imejijengea rekodi ya kutoa huduma salama, za kisasa na zenye ubora kwa watanzania.

Shukrani Kutoka Kwa Uongozi wa Shule

Mkuu wa Shule ya Ihombwe Sekondari, Mwalimu Zackia Hassan Mwangu, ameishukuru Benki ya Stanbic kwa msaada huo muhimu.
Amesema kuwa madawati, viti na miche ya miti vitachangia kwa kiasi kikubwa kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia. Pia ametoa wito kwa watanzania kuiga mfano wa Stanbic katika kuboresha elimu kupitia michango yao ndani na nje ya masomo.

No comments:

Post a Comment