Dar es Salaam, Oktoba 10, 2025 — Kampuni ya Puma Energy Tanzania imeadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja 2025 kwa njia ya kipekee, kwa kuwatembelea na kuwahudumia moja kwa moja wateja katika vituo vyake vya mafuta nchini kote. Wiki hii imeadhimishwa duniani kote kuanzia Oktoba 6 hadi 10, mwaka huu, ikiwa na kauli mbiu ya “INAWEZEKANA”.
Katika shamrashamra hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Bi. Fatma Abdallah, aliongoza wafanyakazi wa kampuni hiyo kushiriki moja kwa moja katika kutoa huduma kwa wateja waliotembelea vituo vyao. Bi. Abdallah alionekana akisaidia kusafisha vioo vya magari, kukagua kiwango cha mafuta ya injini, na hata kujaza mafuta kwenye magari na pikipiki za wateja – kitendo kilichopokelewa kwa furaha na mshangao mkubwa kutoka kwa wateja.
“Wiki ya Huduma kwa Wateja ni wakati muhimu wa kutambua mchango wa wateja wetu. Tunaamini kila mteja ni sehemu ya safari yetu, na ndiyo maana tumeamua kushiriki nao moja kwa moja katika huduma hizi kama ishara ya shukrani yetu kwa uaminifu wao,” alisema Bi. Abdallah.
Aidha, Meneja wa Masoko wa Puma Energy Tanzania, Bi. Lilian Kanora, alishiriki pia kwa kusafisha vioo vya magari ya wateja, huku akisisitiza dhamira ya kampuni hiyo ya kuboresha zaidi huduma na uzoefu wa wateja katika vituo vyake vyote nchini.
Wateja waliotembelea vituo vya Puma Energy katika kipindi hiki walipata zawadi mbalimbali kama sehemu ya shukrani, huku baadhi wakipata nafasi ya kufahamu zaidi kuhusu huduma na bidhaa za kampuni hiyo, ikiwemo Puma Elite Card – kadi maalum inayowawezesha wateja kufanya manunuzi ya bidhaa na huduma zote za Puma Energy kwa urahisi, kufuatilia miamala na matumizi yao popote walipo, bila makato yoyote ya ziada.
Tukio hili limeonyesha kwa vitendo dhamira ya Puma Energy Tanzania katika kujenga uhusiano wa karibu na wateja wake, sambamba na kutoa huduma bora, salama na zenye ubunifu unaoendana na mahitaji ya kisasa ya wateja.
![]() |
| Meneja Masoko wa Puma Energy Tanzania, Bi. Lilian Kanora, akisafisha kioo cha gari la mteja aliyefika kupatiwa huduma katika kituo cha kampuni hiyo. |











No comments:
Post a Comment