Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Tuesday, 14 October 2025

BENKI YA NMB YAPEWA PONGEZI KWA KUTOA ELIMU YA KIFEDHA KWA VIJANA

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Patrobas Katambi, na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera na Uratibu) Zanzibar, Hamza Hassan Juma, wameipongeza Benki ya NMB kwa kuendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali katika kuwawezesha vijana kupitia elimu ya kifedha.

Viongozi hao wametoa pongezi hizo walipotembelea banda la NMB katika Maadhimisho ya Wiki ya Vijana, yanayoendelea katika viwanja vya Soko la Uhindini jijini Mbeya.

Mmekuwa na sapoti kubwa kwa Serikali katika kusaidia elimu ya kifedha kwa vijana. Vijana wengi kwa sasa wamejikwamua kiuchumi kutokana na elimu mnayotoa,” alisema Waziri Katambi.

Kwa upande wake, Waziri Hamza Hassan Juma alisisitiza kuwa vijana wengi wa Kizanzibari sasa wamejikita zaidi katika shughuli za ujasiriamali kutokana na elimu ya kifedha inayotolewa na Benki ya NMB.

Akizungumza wakati akiwakaribisha mawaziri hao, Meneja Mahusiano Mwandamizi wa NMB, Josephine Kulwa, alisema benki hiyo imetumia fursa ya Wiki ya Vijana kutoa elimu ya kifedha kwa makundi mbalimbali ya vijana, ikiwemo wanafunzi wa vyuo vikuu.

Aliongeza kuwa NMB imezindua akaunti maalumu iitwayo Mwanachuo Account, inayowalenga wanafunzi wa elimu ya juu, ambapo wateja wanaotumia huduma ya Mshiko Fasta hupata marejesho ya asilimia 30 ya miamala yao.






No comments:

Post a Comment