Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Monday, 8 September 2025

MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA JKCI: BENKI YA NMB YAPOKEA TUZO MAALUM

Dar es Salaam, Tanzania – Serikali ya Tanzania, kupitia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), imeeleza kuwa imeokoa zaidi ya Shilingi bilioni 172 ambazo awali zingepelekwa kwa wagonjwa wa moyo nje ya nchi. Kauli hii imetolewa jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Albert Msando, kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 10 ya utoaji huduma za matibabu ya moyo kupitia JKCI.


KUOKOA GHARAMA NA KUIMARISHA HUDUMA

Mhe. Msando alisema kuwa kuanzishwa kwa JKCI mwaka 2015 kumewezesha taifa kupunguza gharama kubwa za matibabu nje ya nchi. Aidha, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuwekeza kwenye vifaa vya kisasa vya moyo, vinavyorahisisha huduma na kuendana na teknolojia za kimataifa.

Dk. Peter Kisenge, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, aliongeza kuwa taasisi hiyo imekua hospitali ya rufaa ya kikanda. Wagonjwa kutoka nchi mbalimbali za Afrika na hata nje ya bara wanapata huduma za moyo hapa nchini, jambo linaloonesha mchango wa JKCI katika kuokoa fedha za taifa na kuimarisha sekta ya afya barani Afrika.


NMB BANK: MCHANGO KATIKA SEKTA YA AFYA

Katika hafla hiyo, Benki ya NMB ilitambuliwa na kupokea tuzo maalum kwa mchango wake mkubwa katika kusaidia juhudi za JKCI. Mwaka 2024, NMB na JKCI walisaini makubaliano ya ushirikiano wa Shilingi bilioni 1 kwa kipindi cha miaka minne kusaidia gharama za matibabu ya watoto, sawa na Shilingi milioni 250 kwa mwaka.

NMB Bank imeendelea kuonesha jukumu lake katika maendeleo ya kijamii na kiafya, kwa kushirikiana na wadau muhimu kuboresha maisha ya Watanzania kupitia uwekezaji wa kimkakati katika sekta ya afya.




No comments:

Post a Comment