Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Grooveback Advert_210725

Grooveback Advert_210725

Friday, 11 July 2025

NMB YAZINDUA HUDUMA YA KIDIJITALI YA UNUNUZI NA UUZAJI WA HISA KUPITIA NMB MKONONI

Dar es Salaam – Julai 10, 2025

Benki ya NMB kwa kushirikiana na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) wamezindua rasmi ushirikiano wa kimkakati na wa kidijitali wa ununuzi na uuzaji wa hisa za kampuni mbalimbali zilizoorodheshwa DSE, kupitia huduma mpya inayopatikana ndani ya aplikesheni ya NMB Mkononi.

Huduma hiyo mpya, matokeo ya ubunifu wa muda mrefu kati ya NMB na DSE, inahusisha uunganishaji wa mifumo ya kidijitali ya NMB Mkononi na Hisa Kiganjani, hatua inayowezesha wateja wa NMB kununua, kuuza hisa, kupata taarifa za soko na thamani ya uwekezaji wao kwa urahisi zaidi kupitia simu zao.


TEKNOLOJIA YA KISASA KUWEZESHA USHIRIKI WA KIFEDHA

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bi. Ruth Zaipuna, alisema kuwa huduma hiyo ni hatua kubwa katika kujumuisha Watanzania kwenye masoko ya mitaji kwa njia salama, rahisi na ya kisasa.

“Huduma hii ni matokeo ya ubunifu na ushirikiano baina ya wataalamu wa TEHAMA kutoka NMB na DSE. Wateja sasa wataweza kujisajili, kununua na kuuza hisa, kufanya malipo moja kwa moja kupitia akaunti zao za NMB na kupata taarifa za mwenendo wa soko kwa wakati halisi,” alisema Zaipuna.

Aliongeza kuwa huduma hiyo inathibitisha dhamira ya NMB katika kukuza ushirikishwaji wa kifedha kupitia teknolojia, na inatarajiwa kuongeza kasi ya ushiriki wa Watanzania kwenye sekta ya masoko ya mitaji.


SERIKALI YAIPONGEZA NMB NA DSE

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, aliizindua rasmi huduma hiyo na kupongeza mashirika hayo kwa ubunifu unaoenda sambamba na malengo ya Taifa ya kuimarisha huduma kwa wananchi.

“Huduma hii inachangia moja kwa moja katika maeneo manne muhimu ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa: kuimarisha upatikanaji wa huduma, kubadili mitazamo ya wananchi, kuelimisha jamii kuhusu uwekezaji na kuchochea ushirikiano miongoni mwa taasisi za ndani,” alisema Prof. Mkumbo.

Alisisitiza kuwa huduma hii ni hatua muhimu ya kuhamasisha utamaduni wa kuwekeza miongoni mwa Watanzania, hasa vijana, na kuongeza uelewa kuwa utajiri unaweza pia kupatikana kupitia umiliki wa hisa.


DSE: HATUA MUHIMU KATIKA KUJENGA KESHO BORA

Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE, Peter Nalitolela, alisema huduma hiyo inapanua wigo wa ushiriki wa wananchi katika masoko ya mitaji, na kwamba DSE inajivunia kuwa sehemu ya mabadiliko haya ya kidijitali.

“NMB ni taasisi inayoaminika, na huduma hii ni kielelezo cha dhamira ya pamoja ya kukuza ustawi wa wananchi kupitia fursa za uwekezaji. Wito wetu kwa vijana ni kuanza kuwekeza hata kwa mitaji midogo kwa ajili ya kujenga kesho bora,” alieleza Nalitolela.


CMSA YATAMBUA UBUNIFU NA USHIRIKIANO

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utafiti, Sera na Mipango wa CMSA, CPA Alfred Mkombo, ambaye alimwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA, alitaja huduma hiyo kuwa ni chachu ya maendeleo ya soko la mitaji nchini.

“Huduma hii inatanua fursa za uwekezaji kwa makundi yote ya Watanzania mijini na vijijini. NMB Mkononi inajumuisha zaidi ya wateja milioni 7, na ushirikiano huu umezingatia matakwa ya kikanuni ya CMSA,” alisema Mkombo.

Hafla ya uzinduzi pia ilihudhuriwa na viongozi wengine akiwemo Msajili wa Baraza la Soko la Mitaji na Dhamana, Martin Kolikoli, wakionesha mshikamano wa taasisi katika kuhakikisha Watanzania wanashiriki kikamilifu katika ukuaji wa uchumi kupitia masoko ya mitaji.




No comments:

Post a Comment