Wakulima kutoka Newala na Ruangwa, mkoani Mtwara, wamehitimu mafunzo ya uongezaji thamani wa zao la korosho yaliyoandaliwa na NMB Foundation kwa ushirikiano na Rabo Foundation na kampuni ya Prosperity Agro Industries Ltd.
Akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo hayo, Meneja Mkuu wa NMB Foundation, Nelson Karumuna, alisema kuwa lengo la mafunzo ni kuwajengea wakulima uwezo wa kuongeza thamani ya mazao ili waongeze kipato na kustawi kiuchumi.
Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Newala Alhaji Rajabu Kundya, aliipongeza NMB Foundation na wadau wake kwa jitihada hizo na kusisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na serikali katika kuleta mapinduzi ya kilimo.
Wakulima waliokamilisha mafunzo walikabidhiwa vyeti vya ushiriki, ikiwa ni pamoja na Asha Juta, Laurent Muya, Ismail Chibumbui, Rehema Saidi, na Asha Abrahmani.
Meneja Ubanguaji wa Bodi ya Korosho (CBT), Mangile Malegesi, alisisitiza nafasi ya teknolojia na uongezaji thamani katika kukuza soko la korosho ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Prosperity Agro, Haroun Maarifa, aliwahakikishia wakulima ushirikiano endelevu kwenye uzalishaji na usindikaji.
No comments:
Post a Comment