- Ushindi huu umetokana na ubora, ukubwa, na uongozi wa huduma ya Stanbic Private Banking kwa wateja maalum wa hadhi ya juu (high-net-worth individuals)
- Huduma hii uwapa wateja hawa vigogo masuluhisho ya kifedha ya ziada, ikiwa ni pamoja na ushauri wa kifedha, usimamizi wa mali, uwekezaji, na mikopo ya kipekee
Mafanikio haya yamekuja wakati Benki ya Stanbic ikiadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwake nchini Tanzania. Kwa kipindi hicho, imejijengea heshima kama mshirika anayeaminika katika kutoa huduma za kifedha zenye mwelekeo wa maendeleo, uvumbuzi, na matokeo kwa wateja wake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Stanbic, Manzi Rwegasira, alisema tuzo hiyo inaonesha dhamira ya benki kuendelea kuwa mshirika muhimu wa maendeleo ya taifa. Aliweka wazi kuwa mkakati wa benki unalenga kumuweka mteja katikati ya maamuzi yote ya biashara na kuendeleza huduma zinazoendana na mahitaji ya soko.
Fredrick Max, Mkuu wa Biashara kwa Wateja wa Kibiashara, aliongeza kuwa ushindi huo ni kielelezo cha dhamira ya kusaidia biashara za ndani kufanikisha maendeleo kupitia huduma zilizobuniwa kwa mahitaji yao.
Mbali na Tanzania, Stanbic Group pia ilishinda tuzo za Afrika kwa kuwa Benki Bora ya Wateja Maalum na Benki Bora ya Elimu kwa Wateja katika Global Finance Awards 2025.
Andrei Charniauski wa Euromoney alihitimisha kwa kusema kuwa washindi wa mwaka huu wameweka viwango vipya vya ubora, ubunifu, na uongozi wa huduma za kifedha barani Afrika.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:
Jina: Dickson Senzi
Cheo: Meneja Mwandamizi; Mambo ya Nje, Mawasiliano, na Masuala ya Kampuni.
Barua pepe: Dickson.Senzi@stanbic.co.tz
Kuhusu Benki ya Stanbic, Tanzania
Benki ya Stanbic Tanzania ni mtoa huduma za kifedha anayeongoza nchini Tanzania, anayetoa bidhaa na huduma mbalimbali kwa wateja binafsi, biashara, na mashirika. Kama kampuni tanzu ya Standard Bank Group, Benki ya Stanbic, Tanzania inachanganya maarifa yake ya ndani na uwezo wa kimataifa wa Standard Bank kusaidia ukuaji na maendeleo ya wateja wake.
No comments:
Post a Comment