Dar es Salaam, 3 Aprili 2025: DStv Tanzania inayo furaha kutangaza uzinduzi wa kampeni yake mpya, “Wafalme wa Loko, usikanyage waya”, inayojazwa na burudani za kusisimua na za kipekee. Kampeni hii, imeanza rasmi 3 Aprili, na itaendelea hadi 30 Juni 2025, ikidhihirisha dhamira ya DStv katika kuleta mapinduzi kwenye tasnia ya filamu kwa kuleta maudhui yenye ubora wa hali ya juu na kuwahakikishia watazamaji burudani mpya na ya kuvutia kila wakati.
Kama sehemu ya kampeni ya Wafalme wa Loko, watazamaji watafurahia burudani kadha wa kadha zikiwemo zenye maudhui ya ndani zitakazoonyeshwa kupitia Maisha Magic Bongo DStv ch. (160) kuanzia mapema mwezi huu wa Aprili. Baadhi ya vipindi vinavyosubiriwa kwa hamu ni:
The Makeover – Shindano la kusisimua la urembo linalowashindanisha wasanii bora wa mapambo nchini Tanzania katika safari ya kushindania taji la Best Make-Up Artist. Kipindi hiki kitaanza rasmi Alhamisi, 25 Aprili 2025, saa 2:00 usiku kupitia Maisha Magic Bongo (DStv Channel 160), kikionesha vipaji vya kipekee na ubunifu unaoongoza sekta ya mapambo nchini na kuongozwa na majaji mahiri akiwemo Jacqueline Wolper, Alma Bronxi, Martin Kadinda, Cicie na mtangazaji maarufu Annie Independent.
Jua Kali Season 8 – Tamthilia inayopendwa zaidi inarejea na msimu mpya uliojaa msisimko na visa visivyotabirika. Itaonyeshwa Jumatano hadi Jumapili saa 3:30 usiku kwenye Maisha Magic Bongo (DStv 160).
Mizani ya Ushambega (Msimu Mpya) – Msimu mpya wenye msisimko na mivutano zaidi utaonyeshwa kila Jumamosi saa 1:00 kamili usiku kwenye Maisha Magic Bongo (DStv 160).
Msimu wa Mwisho wa tamthilia ya Huba – Tamthilia inayopendwa na wengi inafikia hitimisho lake kubwa, ikileta mapinduzi ya simulizi mpya, nyuso mpya, zaidi ya drama, vitendo na mapenzi. Itaonyeshwa Jumatatu hadi Ijumaa saa 3:00 usiku kwenye Maisha Magic Bongo (DStv 160).
Ingizo jipya la tamthilia ya Jivu kutoka Showmax – Tamthilia inayosubiriwa kwa hamu inafika kwenye skrini za Tanzania kupitia Maisha Magic Bongo kuanzia 24 Aprili 2025 sambamba na tamthilia ya The Wife yenye mfululizo maarufu wa matukio ya kukata na shoka kutoka Afrika Kusini na kutafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili na utaanza kuonyeshwa kwenye Maisha Magic Bongo kuanzia 25 Aprili 2025.
Ingizo jipya la tamthilia ya Jivu kutoka Showmax – Itakayoanza kuruka rasmi kupitia Maisha Magic Bongo kuanzia 24 Aprili 2025, sambamba na tamthilia ya The Wife, yenya mfululizo wa matukio ya kusisimua kutoka Afrika Kusini, uliotafsiriwa kwa Kiswahili na kuanza kuonekana kupitia Maisha Magic Bongo kuanzia 25 Aprili 2025.
Wateja wa DStv pia wataweza kufuatilia mechi za fainali za soka za ligi kubwa ulimwenguni, vipindi vya watoto, na burudani mbalimbali kwa familia nzima.
"Tunajivunia kuendelea kuwa chachu katika mapinduzi ya tasnia ya filamu hapa nyumbani Tanzania. Mara zote tumekuwa mstari wa mbele katika kuleta kazi zenye ubunifu wa hali ya juu zinazotengenezwa na watanzania, na kampeni ya Wafalme wa Loko inaakisi dhamira yetu ya kuendelea kuunga mkono sekta ya filamu na ubunifu hapa nyumbani," alisema Ronald Shelukindo, Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania. Aliongeza kuwa msimu huu umejaa maudhui ya kuvutia hivyo wateja wa DStv na watanzania kwa ujumla wakae tayari kufurahia burudani mbalimbali kutoka kwa watayarishaji wetu wa hapa hapa nyumbani.
Kwa maelezo zaidi, tembelea www.dstv.com kwa habari na masasisho ya hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment