- Wakulima washukuru kuondokana na makato, kufungiwa akaunti
Akizungumza kwa niaba ya wakulima hao, Makamu Mwenyeki wa AMCOS ya Mwanjelwa, iliyopo wilayani Mbozi, Bw Imani Luvanda alisema kwa kiasi kikubwa wakulima wilayani humo wamekuwa wakiumizwa sana na gharama za makato ya uendeshaji wa akaunti zao za benki pamoja na kufungwa kwa akaunti zao pindi zisipotumika kwa muda kitu ambacho kimekuwa kikisababisha wengi wao kupoteza imani na matumizi ya taasisi rasmi za kifedha.
“Ila sasa kilichotuvutia zaidi kwenye akaunti hii ya NBC Shambani ni kwamba haina makato yoyote ndio kwanza mkulima anapata faida na zaidi haifungwi kiurahisi hadi ipite miaka miwili.Hii kwetu ni habari njema na binafsi takuwa balozi wa kuwaelimisha wenzangu kuhusu kampeni hii na faida za akaunti ya NBC Shambani’’ alisema.
No comments:
Post a Comment