Dar es Salaam, 20 Machi 2025: Benki ya Exim Tanzania, kwa kushirikiana na Mastercard, wamezindua rasmi Kampeni ya UEFA Priceless, mpango kabambe unaolenga kuhamasisha matumizi ya Exim Mastercard huku ikiwapa wateja fursa ya kushinda zawadi ya kipekee. Kampeni hii, itakayodumu hadi Aprili 30, 2025, itawazawadia watumiaji wa Mastercard safari ya kifahari iliyolipiwa kikamilifu kwenda Amboseli, Kenya kwa ajili ya kushuhudia mechi ya fainali za UEFA kupitia usiku wa kipekee wa ‘UEFA Finals Screening Experience’.
Zaidi ya zawadi zinazotolewa, kampeni hii pia inalenga kuimarisha ushirikiano kati ya Mastercard, taasisi za kifedha, wafanyabiashara, na wateja. Kwa kuhimiza njia salama za malipo, mpango huu utawezesha Mastercard kuboresha huduma zake za baadaye na kuimarisha suluhisho za kifedha za kidijitali katika sekta ya fedha inayokua kwa kasi nchini Tanzania.
Kwa upande wake Meneja Mwandamizi wa Masoko na Mawasiliano, Kauthar D’souza kutoka Benki ya Exim, alisisitiza jinsi kampeni hii inavyoleta athari chanya kwa wateja wa benki hiyo. “Sisi kama Benki ya Exim, tunajitahidi kila mara kuwapatia wateja wetu fursa za kipekee zaidi ya huduma za kibenki za kawaida. Kampeni hii inawawezesha wamiliki wa kadi zetu kufurahia manufaa maalum wanapofanya miamala yao ya kila siku. Tunawahimiza wateja wetu wote kushiriki na kupata nafasi ya kushinda safari hii ya kipekee isiyosahaulika.”
Benki ya Exim inaendelea kupanua huduma zake za kifedha kwa njia ya kidijitali, na ushirikiano huu na Mastercard unadhihirisha dhamira yake ya kutoa suluhisho bunifu za kifedha zinazoboresha maisha ya wateja wake. Watumiaji wa Mastercard za Benki ya Exim wanahimizwa kufanya miamala zaidi kwa kutumia kadi zao kabla ya Aprili 30, 2025, ili kupata nafasi ya kushinda safari hii ya kipekee.
No comments:
Post a Comment