Foreign Exchange Rates

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

Monday, 17 February 2025

STANBIC YATANGAZA WASHINDI KATIKA SHINDANO LA "TAP KIBINGWA"

Meneja wa Kadi wa Benki ya Stanbic Tanzania, Irene Mutabihirwa (katikati) akitangaza washindi wa droo ya kwanza ya kampeni ya "Stanbic Tap Kibingwa" ambapo jumla ya washindi watano walipatikana kwa kila moja kujishindia zawadi ya shilingi 500,000. Kampeni hiyo inawezesha wateja kutumia Kadi zao za Visa Debt kwa kufanya malipo mbalimbali ya kidigitali kila siku hadi kufikia milioni 2 kwa mwezi na kuingia kwenye droo hiyo inayoendelea hadi kufikia kilele chake mwezi mwishoni wa mwezi March ambapo droo kubwa itafanyika na mshindi atajishidia gari aina ya Suzuki Fronx. Wengine kwenye picha kushoto ni Irene Kawili, kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania na Kulia ni Meneja wa Huduma Binafsi, Biashara na Masoko wa Benki ya Stanbic, Victoria Kimaro.
  • Washindi watano wamejishindia zawadi ya TZS 500,000 kila mmoja katika droo ya kwanza ya kila mwezi ya Tap Kibingwa, ikiwa ni sehemu mojawapo ya juhudi za kuhamasisha miamala ya malipo kwa njia ya kidijitali.
  • Benki ya Stanbic inaendelea kuwazawadia wateja wake wanaotumia Kadi zao za Visa Debit, huku droo nyingine mbili zikitarajiwa kufanyika mwezi Machi na Aprili mwaka huu.
  • Droo kuu itakayofanyika mwezi Mei, itamzawadia mshindi mmoja gari jipya aina ya Suzuki Fronx, dhamira kuu ya Benki ya Stanbic ni kuwazawadia wateja wake wanaotumia kadi zao kwa kufanya miamala ya kifedha.
Dar es Salaam – Jumatatu, 17 Februari 2025: Benki ya Stanbic imefanya droo ya kwanza ya kila mwezi ya kampeni ijulikanayo kama "Tap Kibingwa", ambapo washindi watano walipokea zawadi ya TZS 500,000 kila mmoja baada ya kutumia Kadi zao za Visa Debit mara nyingi kwa kufanya miamala kwa mwezi wa Januari 2025. Droo hii iliyosimamiwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya Tanzania, ilihakikisha vigezo na kanuni za uendeshaji wa droo ulizingatiwa kwa uwazi.


Kwenye droo hiyo washindi waliotangazwa ni pamoja na Sangwoo Kim, Thomas Alex Nguluma, Dr. Peter Tumbo, Nqobile Memory Ngwenya, na Fardeen Rattansi, ambao wote kwa umoja wao walielezea furaha yao kwa kushiriki katika kampeni hii na kuonyesha jinsi malipo ya kidijitali yanavyokuwa na umuhimu katika shughuli zao za kila siku.

Mimi ni mteja wa benki ya Stanbic kwa miaka mingi na kwa kutumia Kadi yangu ya Visa Debit imekuwa njia rahisi zaidi ya kufanya malipo, hasa ninaposafiri,” alisema Thomas Alex Nguluma. “Kushinda leo ni fursa nzuri kwangu, lakini ushindi halisi ni usalama na urahisi wa malipo kupitia matumizi ya kadi. Sishiki tena fedha nyingi mkononi na nathamini jinsi ninavyofanya miamala yangu kuwa rahisi.”

Mshindi mwingine, Nqobile Memory Ngwenya, alieleza kuwa, “Kufanya malipo kidijitali kumekuwa ni jambo la kawaida kwangu. Iwe ni kununua vitu, kula au kufanya miamala ya kibiashara, Kadi yangu ya Visa Debit inanifanya niweze kulipa kwa urahisi. Ninaishukuru Benki ya Stanbic kwa kuhamasisha mabadiliko haya na kuwafanya watu wengi kujiunga na mfumo wa kidijitali.”

Meneja wa Kadi wa Benki ya Stanbic, Irene Mutabihirwa, ambaye aliongoza hafla hiyo, alisisitiza dhamira ya benki hiyo katika kuendeleza mfumo wa malipo ya kidijitali nchini Tanzania. “Tap Kibingwa siyo kampeni tu, bali ni sehemu ya malengo yetu ya kukuza ubunifu katika sekta ya fedha. Malipo ya kidijitali yana usalama na urahisi, na tunafurahi kuwazawadia wateja wetu kwa kufanya uchaguzi bora wa miamala ya kifedha.

Benki ya Stanbic Tanzania inaendelea kuwa moja ya benki zinazoongoza katika suala la ujumuishaji wa kifedha kupitia kampeni yake ya “Tap Kibingwa,” inayolenga kuwahamasisha wateja kutumia njia za kidijitali kufanya miamala badala ya kutumia fedha taslim. Kadri Tanzania inavyopiga hatua kwenye kuendeleza na kukuza matumizi ya fedha kwa njia ya kidijitali ambao ni salama na yenye ufanisi mkubwa. Malipo ya kidijitali yanaaminika na yanatumika zaidi, kwani yanapunguza hatari zinazohusiana na kubeba pesa taslim kama vile wizi, udanganyifu na usumbufu.

Kwa kuungwa mkono na Benki Kuu ya Tanzania katika kuhamasisha uchumi wa kidijitali, kampeni ya Tap Kibingwa inalenga kuhamasisha matumizi ya Kadi za Visa Debit katika miamala ya kila siku. Kadi ya Visa Debit ya benki Stanbic inatoa suluhisho salama, rahisi, na la kisasa, na kuwawezesha wateja kupata huduma bora za kifedha duniani kote.

Kampeni ya Tap Kibingwa itaendelea hadi Mei 2025, kukiwa na droo nyingine mbili za kila mwezi zitakazofanyika mwezi Machi na Aprili, na hivyo kutoa fursa kwa wateja kuendelea kushinda. Droo kuu ya mwezi Mei itamzawadia mshindi mmoja atakayejishindia gari jipya aina ya Suzuki Fronx, pamoja na safari ya kifahari kwenda visiwani Zanzibar.

Ili kushiriki katika droo zinazofuata, wateja wanahitaji kutumia Kadi zao za Visa Debit za Stanbic kufanya miamala ya TZS milioni 2 au zaidi kwa mwezi. Wateja wanaofanya miamala zaidi TZS milioni 5 au zaidi wataingia kwenye droo hiyo.

Benki ya Stanbic inaendelea kuwa kinara katika kuhamasisha Tanzania kuelekea uchumi wa kidijitali, ikisisitiza usalama wa fedha za wateja wake, miamala rafiki na rahisi, na upatikanaji wa huduma za kifedha za kimataifa. Wateja wanahamasishwa kuendelea kutumia Kadi zao za Visa Debit kwa matumizi ya kila siku na kuwa sehemu ya safari hii ya kuleta mabadiliko katika matumizi fedha kwa njia ya kidijitali.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:

Jina: Dickson Senzi
Cheo: Meneja Mwandamizi; Mawasiliano na Uhusiano
Barua pepe: dickson.senzi@stanbic.co.tz

Kuhusu Benki ya Stanbic Tanzania

Benki ya Stanbic ni shirika linaloongoza katika huduma za kifedha Afrika Mashariki, likijitolea kukuza maendeleo ya kiuchumi na ukuaji katika kanda hiyo. Kupitia suluhisho za kifedha mbalimbali na mkazo mkubwa katika uvumbuzi na huduma inayozingatia mteja, Benki ya Stanbic inasaidia biashara, watu binafsi, na serikali kufikia mafanikio endelevu. www.stanbicbank.co.tz.

No comments:

Post a Comment