Dar es Salaam, Desemba 13, 2024: Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua msimu wa pili wa kampeni yake inayofahamika kama "Tabasamu Tukupe Mashavu," ikilenga kutoa fursa kwa wateja wa benki hiyo kufurahia pamoja na wapendwa wao wakiwemo ndugu, jamaa na marafiki katika Sikukuu za mwisho wa mwaka kupitia punguzo la bei kwenye manunuzi ya huduma mbalimbali.
“Tumeandaa zawadi nyingi na nzuri kwa wateja wetu, ikiwa ni pamoja na safari ya kitalii visiwani Zanzibar iliyolipiwa gharama zote kwa mshindi na mpendwa wake, simu janja zinazotikisa sokoni za Iphone 16 kwa washindi wa kila wiki katika kipindi cha kampeni hii. Lakini pia kuna zawadi nyingine nyingi kama vile gift vouchers, laptops, gas coocker, pesa Taslim na zawadi nyingine tofauti zitakazotolewa kila wiki kwa washindi watakaofanya miamala kwa wingi,’’ alisema.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Meneja Biashara kupitia Kadi, wa Benki hiyo Bi Esnat Hollela alisema ili kushiriki kwenye kampeni hiyo wateja wa benki hiyo wanatakiwa kutumia kadi zao za NBC VISA kufanya miamala kwenye mashine za ATM, Wakala, maduka, vituo vya mafuta,baa, migahawa, Airbnb, safari, hoteli na malipo mbalimbali ya mtandaoni kama vile Netflix, Amazon, na usajili wa mtandaoni.
“Kadri mteja anavyotumia kadi yake na huduma za NBC, ndivyo anavyoongeza nafasi ya kujishindia zawadi. Na kwa mawakala wa NBC na wale wenye mashine za POS za NBC, wanayo nafasi ya kushinda kwa kuongeza idadi ya miamala wanayofanya kwa wateja wao. Kwa mawakala watakaoongeza miamala ya huduma ya NBC Wakala Pesa, watajipatia nafasi ya ushindi kila wiki,’’ alisema
Kwa upande wao kampuni wadau wa kampeni hiyo wakiwemo kampuni ya PUMA Energies, ABC Emperio, GSM, Johari Rotana, Bravo Coco Beach na Numero Uno walisisitiza dhamira yao kupunguza bei kwenye bidhaa zao ikiwa ni sehemu ya ushiriki wao kwenye kampeni hiyo lengo likiwa ni kutoa unafuu kwa wateja wa benki ya NBC kupata fursa ya kufurahia sherehe za mwisho wa mwaka sambamba na wapendwa wao.
No comments:
Post a Comment