Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday 23 September 2024

NI BALAA! VODACOM YATANGAZA WASHINDI WA DROO YA NANE

Mshindi wa nne wa droo kubwa ya kampeni ya Vodacom Tanzania Plc ‘Ni Balaa, Kila Mtu ni Mshindi’ George Thobias (kushoto), akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni ishirini kutoka kwa Meneja Mauzo Mwandamizi Kanda ya Ziwa wa Kampuni hiyo, Victoria Ngoya (kulia), katika Duka la Vodacom lililopo Jijini Mwanza mwishoni mwa wiki iliyopita. George pia amepata nafasi ya kuchagua shule anayotaka na kisha Vodacom wataenda kukarabati maktaba ya shule hiyo. Ili kuibuka mshindi endelea kufanya miala mingi. Ni Balaa!
Meneja wa duka la Vodacom jijini Mwanza, Jumeo Iddi (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni moja mshindi wa droo ya nane ya Kampeni ya Ni Balaa, Kila Mtu ni Mshindi Bw. Seleman Benjamin (kulia) katika hafla iliyofanyika dukani hapo mwishoni mwa wiki iliyopita. Ili kuibuka mshindi endelea kufanya miamala kwa kutumia M-Pesa super App au kununua vifurushi kwa kupiga *150*00#
Ni Balaa! mshindi wa droo ya nane ya kampeni ya Ni Balaa, Kila Mtu Ni Mshindi kutoka Vodacom Tanzania Plc, Bi. Proscovia Johnbosco (kushoto), akipokea mfano wa hundi ya Shilingi milioni moja kutoka kwa Meneja Mauzo wa mkoa wa Mwanza, Gift Tesha (kulia) katika Duka la Vodacom lililopo Jijini humo mwishoni mwa wiki iliyopita. Kupitia kampeni hii wateja wa Vodacom wanajiongezea nafasi za kushinda kila wakinunua vifurushi au kufanya miamala kupitia M-pesa Super App.

No comments:

Post a Comment