Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB, Adam Mihayo amesema Mkataba huu wa makubaliano unathibitisha dhamira ya Benki ya TCB kuwezesha uchumi jumuishi na maendeleo ya kiuchumi kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa ZEEA, Juma Burhan Mohamed amesema wanalenga kuipatia Benki ya TCB kiasi cha shilingi bilioni 1.8 ili waanze utoaji wa mikopo hiyo ambayo itarejeshwa kwa kipindi cha miaka 2.
Lengo la mikopo hiyo ikiwa ni kuvifikia vikundi 75 vyenye wanachama kati ya watano (5) mpaka ishirini (20), ZEEA mpaka sasa imeshasajili vikundi 16 kutoka sekta mtambuka na kupokea maombi ya mkopo yanayofikia wastani wa shilingi milioni 150.
Kwa kutoa mikopo nafuu kwa makundi haya, TCB na Mpango huu wa mikopo umekusudiwa kutia chachu juhudi za kijasiriamali, kuwapa wajasiriamali uthubutu wa kuanzisha na kupanua biashara zao. Malengo ya uwezeshaji huu ni kuwa chanzo cha mabadiliko mengine kama kuimarisha biashara na uchumi.
No comments:
Post a Comment