Kwa mara ya kwanza nchini, tumezindua rasmi NMB Jiwekee, yenye lengo la kuhifadhi pesa kidijitali kwa ajili ya maisha ya baadae.
Kupitia NMB Jiwekee, mteja ataweza:
- Kuweka kati ya asilimia 1-100 ya kipato kinachoingia kwenye akaunti yake na anaweza kubadilisha muda wowote
- Kuhifadhi hela kwenye NMB Jiwekee kuanzia miaka 5 na kuendelea
- Kuvuna riba shindani na ataipata kila baada ya miezi mitatu
- Kusitisha uchangiaji kwa muda kutokana na mahitaji, bila ya kutoa pesa zake kwenye NMB Jiwekee, na ataweza kuendeleza uchangiaji wakati wowote kupitia NMB Mkononi
- Hakuna kiingilio wala makato
- Kuweka amana katika NMB Jiwekee kupitia mitandao ya simu, benki zingine na mifumo yetu yote
- Kuangalia salio na taarifa za michango yako kupitia NMB Mkononi
Pia, mahojiano yaliongozwa na @millardayo huku mada za utunzaji pesa zikitolewa na @lamataleah pamoja na @masoudkipanya.
No comments:
Post a Comment