Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja (kulia), akifafanua jambo wakati wa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NCBA Tanzania Bw. Claver Serumaga (hawapo pichani), ulioangazia ushirikiano wa maendeleo. |
Mkuu wa masuala ya Biashara wa Benki ya NCBA Tanzania, Bw. Godson Biyengo, akieleza mpango wa maendeleo wa Benki yake wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NCBA Tanzania Bw. Claver Serumaga (kushoto), ulioangazia ushirikiano wa maendeleo, katika Ofisi ya Waziri wa Fedha Treasure Square, jijini Dodoma. Kulia ni Mkuu wa masuala ya sekta ya umma wa Benki hiyo, Bi. Judy Mkama. |
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia) akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NCBA Tanzania Bw. Claver Serumaga, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo kuhusu ushirikiano kati ya Benki hiyo na Serikali katika kuchangia maendeleo, katika Ofisi ya Waziri wa Fedha Treasure Square, jijini Dodoma. |
No comments:
Post a Comment