Dodoma, 11 Mei 2024: Exim Bank imeshirikiana na Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS) pamoja na Mpango wa Damu Salama Tanzania (NTBS) kupanda miti na kuendesha zoezi la uchangiaji damu katika maadhimisho ya Siku ya Msalaba Mwekundu Duniani yaliyofanyika jijini Dodoma ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Dkt Dotto Biteko, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.
“Mwaka jana tulishirikiana na Mpango wa Damu Salama Tanzania (NTBS) kuratibu zoezi la uchangiaji damu katika mikoa ya Mbeya, Mtwara, Mwanza, Dar es Salaam na hapa Dodoma ambapo tulitambuliwa na Serikali kama moja ya wadau wakuu katika zoezi la uchangiaji damu hapa nchini,” anafafanua Stanley.
Mwaka huu, Exim bank imeendelea kushirikiana na Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania katika maadhimisho hayo yenye kaulimbiu ya "Natoa kwa furaha, na furaha ninayotoa ni zawadi." ikisisitiza umuhimu wa kujitoa ajili ya afya njema kwa wenye mahitaji na furaha inayoambatana na kitendo hicho kwa pande zote mbili kwa mtoaji na mpokeaji.
No comments:
Post a Comment