Mgeni rasmi katika shughuli hiyo Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii - Dk. Hassan Abbas aliipongeza Benki ya NMB kwa kuja na programu hii ambayo pia inasapoti Serikali katika kuipa thamani zaidi Kampeni ya Achia Shoka, Kamata Mzinga na hivi karibuni, Serikali imeiinginza sekta ya asali na nyuki katika Programu ya Kujenga Kesho Iliyo Bora kwa Vijana na Wanawake nchini (BBT). Lakini pia, juhudi hizi ni sehemu ya maandalizi ya Serkali kuelekea Mkutano Mkuu wa Wafugaji Nyuki Duniani utakaofanyika Tanzania mwaka 2027, ambao utawahusisha waataalum wakimataifa zaidi ya 4,000.
Dkt. Abbas alisisitiza kuwa Tanzania ina mazingira mazuri ya uzalishaji wa mazao ya nyuki yenye kiwango cha juu cha ubora kutokana na uwepo wa misitu yenye mimea inayotoa chakula kwa nyuki huku sekta hiyo ikichangia ajira zaidi ya watu milioni mbili na kukadiliwa kuwa na uwezo wa uzalishaji wa asali tani 138,000 kwa mwaka.
Kamishna wa Uhifadi Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Profesa Dos Santos Silayo amesema Benki ya NMB imekuwa na ushirikiano nao katika utunzaji mazingira na upandaji miti tangu mwaka 2022 kupitia kampeni yao ya Miti Milioni na anawashukuru sana.
No comments:
Post a Comment