Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji anaemaliza muda wake Mark Ocitti na Mkurugenzi Mtendaji mpya. |
Kampuni hiyo pia inapanga kuongeza udahili wa wanafunzi kutoka nchi zenye uhitaji wanaosomea kozi za stashahada ya kilimo chini ya mpango wake wa ufadhili unaoitwa ‘Kilimo Viwanda’ ambao umewanufaisha zaidi ya wanafunzi 230 katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Bw. Ocitti.
Ocitti aliyasema hayo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika hafla ya kumuaga kwani kampuni mama ya SBL ya Diageo imemteua kuhama na kuiongoza kampuni ya bia ya Kenya Breweries, kampuni ndugu ya SBL.
Ocitti aliongoza SBL kwa kipindi cha miaka mitatu, ikiwa ni pamoja na viwanda vya uzalishaji bia vya Dar es Salaam, Moshi na Mwanza. Katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Ocitti SBL, kampuni hiyo imepata mafanikio makubwa, ikiwa ni pamoja na kuzindua mradi wa upanuzi wa kiwanda chake cha Moshi.
Akizungumza katika hafla ya kumuaga Ocitti, naibu waziri wa viwanda na biashara, Exaud Kigahe amempongeza Ocitti kwa mchango wake katika kukuza sekta ya viwanda nchini Tanzania kupitia uchapakazi wake, kujituma na uadilifu, “kwa miaka 3 iliyopita Bw.Ocitti amekuwa pamoja nasi hapa nchini, amedhihirisha kuwa yeye ni kiongozi mwenye maono, ambaye alitaka kuipeleka SBL juu zaidi, na hii sio kwa SBL tu kama kampuni ila pamoja na wafanyakazi wa SBL.”
Naibu waziri hasa, alimpongeza Ocitti kwa kusimamia utekelezaji wa kiwanda cha kwanza kabisa cha uzalishaji wa pombe kali mjini Moshi ambacho kinaendeshwa na wanawake kwa asilimia mia.” Nafahamu kwamba moja ya nguzo za SBL ni ujumuishaji na Bw. Ocitti ametekeleza hili kwa kiasi kikubwa, kwa mara ya kwanza katika nchi yetu, tuna kiwanda kinachoendeshwa na wanawake tu na hiii ni kutokana na kujidhatiti kwa Ocitti kwenye swala la ujumuishi.” Aidha Naibu Waziri huyo alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji aliyemaliza muda wake kwa kusimamia uzinduzi wa mtambo wa upanuzi wa SBL mjini Moshi, akibainisha kuwa ni kupitia uongozi wa Ocitti mradi huo ulifanikiwa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya SBL, John Ulanga alitoa shukrani zake kwa Ocitti kwa niaba ya bodi ya Wakurugenzi wa SBL, akibainisha mafanikio ya Ocitti SBL, “katika miaka 3 tu ambayo SBL ilikuwa ikiongozwa na Bw. Ocitti, naweza kusema kwa ujasiri kwamba ameleta mafanikio mengi SBL, mafanikio ya kibiashara na kwa jamii ya Watanzania kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo ya jamii ambayo ameisimamia kwa hali na mali, kuanzia miradi ya maji, elimu na miradi ya kuwawezesha wakulima.”
Katika hafla ya kumuaga, SBL ilimtambulisha Mkurugenzi Mtendaji wake mpya, Obinna Anyalebechi ambaye anajiunga na biashara hiyo kutoka Diageo London.
No comments:
Post a Comment