Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Tabia Maulid Mwita (katikati waliosimama) akishuhudia utiaji saini wa mkataba wa ushirikiano wa kibiashara na udhamini kwa timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Zanzibar (Zanzibar Heroes), kati ya Benki ya CRDB iliyowakilishwa na Afisa Mkuu wa Biashara, Boma Raballa (kulia) Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) lililowakilishwa na Rais wake, Abdullatif Ali Yassin (katikati) pamoja na Kampuni ya Ubunifu wa Mavazi ya Sheria Ngowi chini ya Sheria Ngowi mwenyewe (kushoto). Udhamini huo ni wa utengenezaji wa Jezi na Vifaa vya Michezo kwa Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kwa muda wa miaka 5, na Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), pamoja na Kampuni ya Ubunifu wa Mavazi ya Sheria Ngowi. Hafla ya kusaini mikataba hiyo imefanyika Machi 17, 2023 kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar. Wengine pichani ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), Hafidh Mohamed Ali (wa pili kushoto waliosimama), Katibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), Hussein Ahmada Vuai pamoja na Wanasheria. |
No comments:
Post a Comment