Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday 13 February 2023

ENGEN NA VIVO ENERGY WAUNGANA KUKUA KIBIASHARA BARANI AFRIKA


Cape Town, Afrika Kusini: Kampuni maarufu za usambazaji wa nishati na vilainishi, Engen na Vivo Energy zimetangaza kuungana na hivyo kutengeneza ushirika mkubwa wa usambazaji wa bidhaa hizo barani Afrika.

Kwa kuungana kwao kumefanya wawe na uwezo wa pamoja wa vituo vya huduma 3,900 na uwezo wa kuhifadhi lita bilioni mbili katika nchi mbalimbali za Bara la Afrika. Kampuni hizo zinafanya shughuli zao katika nchi 27 za Afrika.

Engen ambayo ni maarufu nchini Afrika Kusini ina vituo vya huduma 1,300 katika nchi saba za Afrika, huku Vivo Energy ikiwa kampuni kubwa ya usambazaji wa mafuta na vilainishi ina vituo zaidi ya 2,600 katika nchi 23wakitumia alama (nembo) ya Engen na Shell.

Katika muunganiko huo kampuni ya Petronas itauza hisa zake asilimia 74 zilizopo katika kampuni ya Engen kwa Vivo Energy na kampuni ya Phembani Group, mshirika wa karibu wa Petronas barani Afrika na mwenye hisa kwenye kampuni ya Engen ya B-BBEE ataendelea kuwa na uhusiano na Engen kwa kuendelea kuwekeza asilimia 21 ya biashara zake nchini Afrika Kusini.

Muunganiko huo utawanufaisha waajiriwa wa Engen ambao kupitia mpango maalumu wa asilimia tano wa umiliki wa kampuni wa wafanyakazi unafanya asilimia 26 kumilikiwa na watu ambao awali hawakuwa wanatarajiwa.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Vivo Energy, Stan Mittelman anasema kwamba nia ya kampuni yake ni kuwekeza zaidi katika kukua kibiashara na kwamba tangu ianzishwe mwaka 2011 wameongeza uwezo wao mara mbili zaidi.

“Miaka minne iliyopita tulinunua soko la Engen katika nchi nane za Afrika na tumeendelea kuhakikisha kwamba tunakuza na tunakua kibiashara. Kumilikiwa kwa Vivo Energy kwa asilimia 100 na Vitol mwaka jana, kulifanya kampuni ikue kwa kasi zaidi. Makubaliano yatakapofikia mwisho katika utekelezaji wa kuunganika kwa Vivo Energy na Engen tutakuwa tumepiga hatua kubwa zaidi katika soko la Afrika Kusini na masoko mengine muhimu,” alisema Mittelman.

Naye Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mkuu wa Engen, Seelan Naidoo alisema kuunganika kwao na Vivo kunatoa mwanga mpya katika utendaji wa kazi zao na hasa kuendelea kuwa vinara katika soko la Afrika Kusini na mataifa mengine ya Afrika.

Phuthuma Nhleko, Mwenyekiti na mwanzilishi mwenza wa Phembani Group alisema wanajisifu sana kwa kuiwezesha Engen kukua na kwamba sasa wanajisikia fahari kuunganika na Vivo Energy katika ukuaji wa kampuni hizo.

Mwenyekiti wa Vivo Energy, Chris Bake amesema kwamba kampuni hiyo imeendelea kufanya vyema tangu kuanzishwa kwake na kwamba ina wataalamu na menejimenti imara yenye muono na ubunifu kuwezesha kukua na kuhudumia masoko yake muhimu likiwemo la Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment