Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa kwanza kulia) akimwelezea Balozi wa Denmark nchini, Mette Nørgaard Dissing-Spandet (wa pili kushoto) juu ya Mkakati mpya wa Miaka Mitano wa Biashara wa Benki ya CRDB wa 2023/2028 wakati ujumbe wa Benki hiyo ulipotembelea katika Ubalozi wa Denmark kujadili mafanikio ya uwekezaji wa DANIDA ndani ya benki hiyo. Ujumbe huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay (wa pili kulia), pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Prof. Neema Mori (hayupo pichani), Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (wa tatu kushoto), na Katibu wa Kampuni Benki ya CRDB, John Rugambo.
Hakuna wakati mzuri wa kujadili uhusiano huo wa kihistoria kama kipindi hiki ambacho benki hiyo kinara wa utoaji huduma za kifedha nchini, imetoka kupata faida kubwa kwa mwaka uliopita.
Ikiivunja rekodi yake yenyewe iliyoiweka kwa mwaka 2021 ya faida baada ya kodi ya takriban Sh268 bilioni na kufikia faida ya Sh353 bilioni kwa mwaka 2022.
Mafanikio hayo yanaelezwa kutokana na jitihada za makusudi za benki hiyo kukuza vyanzo vya mapato yasiyotokana na riba ambapo yaliongezeka kwa asilimia 13 mwaka hadi mwaka na kufikia kiasi cha Sh400 bilioni kutoka Sh354 bilioni.
Nsekela, akifafanua rekodi hiyo, alisema imechagiwa na ongezeko la ufanyaji miamala ya fedha hususan kupitia njia za kidijitali.
Kiujumla, wanahisa wa benki hii, DANIDA akiwa mmojawapo akishirikiana na Serikali ya Tanzania, wanaendelea kuona fahari ya kuwa sehemu ya uwekezaji wa benki inayofanya vizuri kwa kuwa wana uhakika.
No comments:
Post a Comment