Kitomari Banking & Finance Blog is a premier site for banking, finance, business, economic, investment and stock market news as well as selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the World. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.
Friday, 20 January 2023
WAZIRI MABULA AZINDUA BODI MPYA YA NHC AKISISITIZA UJENZI WA KASI WA KISASA
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk. Angeline Mabula ameiagiza Bodi mpya ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa ihakikishe inachochea ujenzi wa kisasa unaotumia teknolojia zinazowezesha ujenzi wa kasi, wenye gharama nafuu na unaowawezesha walaji kupata thamani ya fedha zao (value for money) ili kuweza kumudu ushindani katika soko.
Ameyasema hayo wakati akizindua Bodi Mpya ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba la Taifa uliofanyika kwenye hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha jana.
“Niwaombe mhakikishe mnasimamia ipasavyo suala la ubunifu hususan katika matumizi ya teknolojia zinazowezesha ujenzi wa kasi, wenye gharama nafuu na unaowawezesha walaji kupata thamani ya fedha zao (value for money) ili kuweza kumudu ushindani katika soko,”amesema.
Amesisitiza Shirika liwekeze kwenye miradi yenye tija ambayo imefanyiwa upembuzi yakinifu (feasibility study) kitaalamu ili kuepusha kuwekeza fedha za umma kwenye miradi isiyo na tija na yenye kuliletea Taifa hasara.
Ameielekeza bodi hiyo ihakikishe Shirika linaongeza uwezo na idadi ya miradi ya kandarasi za ujenzi ili kuliwezesha kuongeza mapato kwa ajili ya kujiendesha na utekelezaji wa miradi ya uendelezaji milki.
“Jukumu la Usimamizi sahihi wa majengo (property management) ni jambo la msingi katika kuhakikisha utunzaji wa thamani za rasilimali hizo na kupunguza gharama kubwa zinazotokana na majengo kutosimamiwa ipasavyo hususan suala la matengenezo (maintenance), ukarabati (repair) na matumizi sahihi ya majengo,”amesema.
Amewapongeza wajumbe wote mlioteuliwa kushiriki katika kulisimamia Shirika la Nyumba la Taifa kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Naye Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Sophia Kongela amemshukuru Waziri na serikali kwa kuendelea kuliunga mkono Shirika na kwamba Bodi yake itaendelea kuhakikisha kuwa maelekezo yote ya Serikali yanaenda kutekelezwa na Bodi.
Bodi hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Sophia Kongela na Novemba Mosi, 2022 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angeline Mabula kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 5(2) cha Sheria Na. 2 ya Mwaka 1990, akawateua Wajumbe 7 wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa. Aidha, uteuzi huu ambao ni wa kipindi cha miaka mitatu (3), kuanzia tarehe 01 Novemba, 2022.
Wajumbe wa Bodi hiyo ni Johnny Kalupale, Eliud Sanga, Frank G.H Hawasi, Profesa Wilbard Kombe, Dorothy Mwanyika, Charles Singili na Tausi Mbaga Kida.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment