Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 20 January 2023

TANZANIA COMMERCIAL BANK YASHIRIKI UZINDUZI UJENZI WA RELI YA KISASA KUTOKA TABORA HADI ISAKA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango akisikiliza maelezo ya ushiriki wa Benki ya TCB (Tanzania Commercial Bank) katika ujenzi wa Reli ya Kisasa(SGR) kutoka kwa Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Adolphina William wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa reli ya SGR LOT 4 kati ya Tabora na Isaka, uliofanyika mjini Isaka, mkoani Shinyanga.

Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Adolphina William (kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa reli ya SGR LOT 4 kati ya Tabora na Isaka, uliofanyika mjini Isaka, mkoani Shinyanga ambapo katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango.


Tanzania Commercial Bank (TCB) Imeendelea kushiriki zoezi endelevu la ujenzi wa kipande cha nne cha ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Tabora hadi Isaka chenye urefu wa kilomita 165.

TCB imeshirikia kikamilifu katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha kutoka Tabora hadi Isaka chenye urefu wa kilomita 165.

TCB imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo katika sekta mbalimbali na kuhakikisha kuwa inatoa huduma stahiki kila kona ya Tanzania na kuhakikisha inaunga mkono kwa asilimia zote maendeleo ya nchi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa wateja wakubwa wa Tanzania Commercial Bank Adolphina William wakati wa uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa reli ya Kisasa (SGR) awamu ya nne leo Mkoani Shinyanga

Adolphina amesema, Tanzania Commercial Bank ni Benki ya Wananchi na wamejitoa na wameshiriki kwa hatua kubwa katika kuhakikisha shirika la Reli Tanzania (TRC) linafanikisha mradi wa SGR kwa mafanikio makubwa.

“Tanzania commercial Bank ni wadau wakubwa wa maendeleo hapa nchini na kuchangia ujenzi wa Taifa, TRC wanafanya kazi nzuri sana kuhakikisha wanaunganisha wananchi kwa njia ya usafiri wa reli hivyo mradi huu wa SGR utaleta mafanikio makubwa hapa nchini.

Adolphina ameeleza kuwa kwa Sasa Tanzania Commercial Bank ina matawi kila pembe ya Tanzania hivyo imejipanga vyema kutoa huduma kwa watanzania pamoja na wageni kutoka nje hivyo amewasihi watanzania ambao bado hawajafungua akaunti na benki ya TCB wakafungue akaunti ili kunufaika na huduma zinazopatikana katika Benki hiyo.

No comments:

Post a Comment