Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Monday 19 December 2022

DStv YAJA NA OFA KABAMBE MSIMU HUU WA SIKUKUU


  • Ukilipia kifurushi chako unapewa cha juu yake bila malipo ya ziada
Kama kawaida DStv haiwaachi wateja wake mikono mitupu msimu wa sikukuu! Msimu huu wateja wote wa DStv wanapata mserereko ambapo kuanzia tarehe 19 Desemba 2022 hadi 24 Janunari 2023 mteja wa DStv atakayelipia kifurushi chake atapandishwa nakuunganishiwa kifurushi cha juu yake kwa mwezi mzima bila malipo ya ziada.

Akitangaza kuzinduliwa kwa kampeni hiyo ya msimu wa sikukuu, Mkuu wa thamani kwa wateja wa MultiChoice Tanzania, Hilda Nakajumo amesema kuwa ofa hii ni kwa wateja wote wa DStv watakaolipia vifurushi vyao katika kipindi hicho ambapo DStv itawatunuku kifurushi cha juu yake bila malipo ya ziada.

Amesema hata kama mteja kifurushi chake kilimalizika na alikuwa hajalipia, atapata ofa hiyo punde tu atakapo huisha kifurushi chake cha awali.

“Msimu huu wa sikukuu tunaileta familia ndugu na jamaa pamoja ili kuhakikisha kuwa hawapungukiwi na burudani, tumeamua kuwazawadia ofa hii kabambe ili kuwawezesha kupata burudani ya hali ya juu kwa kufurahia chaneli nyingi Zaidi za DStv zikiwemo katuni kwa ajili ya Watoto, michezo, tamthilia, habari na makala mbalimbali”, alisema Hilda.

Hilda amesisitiza kuwa wateja wa Compact Plus ambao watapandishwa mpaka kwenye kifurushi cha Premium wataweza kufuruhia sikukuu hii pamoja na wapenzi wao huku wakiangalia vipindi pendwa zaidi ndani ya DStv. Kuna msimu mpya wa tamthilia pendwa ya 'The Good Doctor' kuanzia tarehe 5 Desemba mwaka huu ndani ya M-Net pamoja na filamu maarufu kila Jumapili kama The King’s Man, The Bad Boys pamoja na Moonfall.

Mteja anayelipia kifurushi cha Compact atapandishwa mpaka kwenye kifurushi cha Compact Plus ambapo ataweza kufurahia vipindi kama Real Housewives of Salt Lake City ndani ya Magic kuanzia tarehe 26 Desemba na pia atajionea msimu mpya wa The History of Christianity ndani ya chaneli ya Curiosity kuanzia tarehe 25 Disemba.

Wateja wa kufurushi cha Shangwe watapandishwa kwenye kifurushi cha Compact ambapo watafurahia vipindi kama The Best Man Holiday kuanzia tarehe 25 Desemba, kipindi maarufu cha Trevor Noah: Welcome to America kuanzia tarehe 18 Desemba pamoja na Mad Madea Week ndani ya Studio Universal kuanzia tarehe 12 Desemba.

“Msimu wa sikukuu familia nyingi zinakutana pamoja na hawa ndio wapenzi wetu. Tunataka wateja wetu washerehekee sikukuu kwa furaha zaidi kwa kupata burudani isiyo kifani kupitia DStv. Kwa kuwa msimu huu ni msimu wa kutoa, basi na sisi tumeona tutoe kwa wateja wetu ili waweze kuunganika na wapenzi wao kwa kutengeneza kumbukumbu pamoja na DStv”

Kwa taarifa zaidi juu za ofa hii kabambe pamoja na vipindi pendwa unavyoweza kuangalia ndani ya DStv, tembelea www.dstvafrica.com. Pia unaweza kupakua progamu ya MyDStv App ili uweze kujihudumia kiurahisi ili kuhakikisha unapata huduma popote ulipo kipindi hiki cha sikukuu.

No comments:

Post a Comment