Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango akishuhudia burudani ya ngoma za asili alipowasili kwenye hafla hiyo. |
Akizungumza kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo za 16 za Rais kwa vinara wa Uzalishaji viwandani (PMAYA) iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Dkt Mpango aliemuwakilisha Rais Samia Suluhu alisema mchango wa taasisi za kifedha ni muhimu katika kukuza sekta ya viwanda na kuongeza ushindani katika soko la ndani na nje ya nchini.
“Kama ambavyo wadau wenyewe wa sekta ya viwanda wanavyowaita Benki ya NBC mshirika muhimu wa sekta ya Viwanda nami pia kwa niaba ya serikali nawapongeza NBC pamoja na wadau wengine wote kwa kuwa pamoja na sekta hii muhimu.’’
Baadhi ya maofisa waandamizi wa Benki ya NBC pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya viwanda nchini wakifuatilia hafla hiyo. |
“Mchango wenu ni muhimu sana ninaomba sana ushirikiano huu uendelee zaidi kwasababu sekta ya viwanda inategemea zaidi huduma nzuri za kifedha…hongereni sana NBC,’’ aliipongeza benki hiyo iliyokuwa mdhamini mkuu wa tuzo hizo.
Baadhi ya maofisa waandamizi wa Benki ya NBC pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya viwanda nchini wakifuatilia hafla hiyo. |
Awali akizungumza kwenye hafla ya tuzo hizo zilizoratibwa na Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi alisema mafanikio makubwa ambayo benki hiyo inayapata kwa kiasi kikubwa yanachagizwa na dhamira thabiti pamoja na jitihada za serikali katika kujenga Tanzania inayoondeshwa na uchumi wa Viwanda na Biashara.
“Ushiriki wa Benki ya NBC kwenye matukio kama haya yanayowakutanisha wadau wa sekta ya viwanda nchini yanatupa ufahari sana kwa kuwa yanatukutanisha na wadau wetu muhimu wote tukiwa na dhamira moja kuu ambayo ni kuongeza ukuaji wa uchumi na ushindani wenye tija kwa faida ya taifa letu. Tunawashukuru sana Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI) kwa kutuona NBC kama wadau sahihi katika kufanikisha tuzo hizi muhimu,’’ alisema.
Kwa mujibu wa Bw Sabi, kupitia uwekezaji mkubwa katika huduma za Kidigitali, benki hiyo kwasasa imefanikiwa kurahisisha utoaji wa huduma zake kwa wateja wote wakiwemo wamiliki wa viwanda ambao kwasasa hawalazimiki kutembelea matawi ya benki hiyo ili kupata huduma kwa kuwa wanaweza kukamilisha huduma zote muhimu za benki hiyo wakiwa kwenye biashara zao kupitia huduma za kidigitali.
“Mbali na ufanisi katika utoaji wa huduma pia tunajivunia ushirikiano wetu na wadau wote wakubwa na wadogo kibiashara kupitia ‘NBC Biashara Clubs’ zilizopo maeneo mbalimbali nchini. Kupitia klabu hizi tumeweza kuwajengea uwezo wa kibiashara wadau hawa kupitia semina za mafunzo, kuwasogezea huduma za kibenki, kuwajengea mitandao ya kibiashara pamoja na kuwapa mbinu za kurasimisha biashara zao ili waweze kukopesheka.’’ Alisema.
Aidha Bw Sabi alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wadau hao wa viwanda kuhakikisha wanachangamkia fursa ya kuwekeza kwenye Hati Fungani ya NBC Twiga Bond ili waweze kunufaika na faida mbalimbali zitokazo na Hati fungani hiyo.
“Kiasi cha chini cha ununuzi wa hati fungani hiyo ni TZS 500,000. Kupitia uwekezaji huu wahusika wataweza kupata riba kubwa ya 10% kwa mwaka, inayolipwa nusu mwaka katika kipindi chote cha miaka mitano hadi Novemba 2027. Kiwango cha riba kinacholipwa hakina punguzo la kodi. Hivyo nawakaribisha sana wadau wa viwanda kwenye uwekezaji huu ambao pamoja na mambo mengine unalenga kukuza sekta ya uzalishaji kupitia viwanda vidogo vidogo,’’ Alisema.
No comments:
Post a Comment