Akizungumza katika hafla ya kutangaza udhamini huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema benki hiyo imeendelea na uamuzi wake wa kudhamini ligi hiyo ya taifa ya mpira wa kikapu kwa mara ya tatu mfululizo ikiwa ni sehemu ya jitihada za benki hiyo kuwawezesha vijana wa Kitanzania kupitia michezo.
Aliongeza kuwa Benki ya CRDB kupitia Sera yake ya Uwekezaji katika Jamii (CSI Policy) imekuwa ikiwekeza katika michezo ya vijana kwa kuamini kuwa inasaidia kuongeza ushiriki wao katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika jamii.
“Kupitia mashindano haya mbali na kuonyesha vipaji vyao, pia wamekuwa wakipata scholarship za masomo, na kupata mafunzo mbalimbali ambayo yanasaidia kuwajengea kujiamini, kujisimamia na kuzifuata ndoto zao,” alisema Nsekela huku akiishukuru kampuni ya Sanlam kwa kuendelea kuunga mkono mashindano hayo.
“Pamoja na zawadi hizi za timu kutakua na zawadi kwa wachezaji bora wa maeneo mbalimbali na makocha. Jumla ya zawadi zote za fedha taslimu zilizotengwa mwaka huu ni Shilingi milioni 32. Lakini hapo baadae tutakwenda kutangaza zawadi nyengine za ufadhili wa masomo kwa wachezaji watakaofanya vizuri na mwaka huu tutaboresha zaidi,” aliongezea.
Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa CRDB Bank Taifa Cup 2022, Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mchezaji wa Mpira wa Kikapu, Esther Matiko aliipongeza Benki ya CRDB kwa kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kusaidia jitihada za serikali kuendeleza michezo nchini.
Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania(TBF), Michael Kadebe aliishukuru Benki ya CRDB na Sanlam kwa kuendelea na udhamini wa ligi hiyo huku akibainisha kuwa udhamini wa taasisi hizo kubwa hapa nchini umesaidia kuongeza hamasa na mapenzi ya mpira wa kikapu kwa vijana kama ilivyo kwa mpira wa miguu na michezo mingine.
Hafla ya kutangaza udhamini kwa mwaka 2022 ilienda sambamba na mtanange mkali wa timu za wachezaji bora kwa mwaka 2020 na 2021 kwa upande wa wanawake na wanaume. Aidha katika hafla hiyo pia kulichezeshwa droo ya makundi ambapo timu 20 za wanaume na 16 zitachuana vikali.
Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa CRDB Bank Taifa Cup 2022, Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mchezaji wa Mpira wa Kikapu, Esther Matiko akiongoza uchezeshaji wa droo ya Mashindano ya CRDB Bank Taifa Cup 2022 wakati wa ufunguzi rasmi wa msimu wake wa tatu, ulioenda sambamba na mchezo maalumu uliowakutanisha wachezaji waliokuwa bora katika 'CRDB Bank Taifa Cup 2020 na 2021' (MVPs) uliochezwa jana kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay, jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Bodi ya Benki ya CRDB, Martin Warioba akishiriki uchezeshaji wa droo ya Mashindano ya CRDB Bank Taifa Cup 2022 wakati wa ufunguzi rasmi wa msimu wake wa tatu, ulioenda sambamba na mchezo maalumu uliowakutanisha wachezaji waliokuwa bora katika 'CRDB Bank Taifa Cup 2020 na 2021' (MVPs) uliochezwa jana kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay, jijini Dar es salaam.
Meneja wa kampuni ya bima ya Sanlam Life Assurance, Killian Nango akishiriki uchezeshaji wa droo ya Mashindano ya CRDB Bank Taifa Cup 2022 wakati wa ufunguzi rasmi wa msimu wake wa tatu, ulioenda sambamba na mchezo maalumu uliowakutanisha wachezaji waliokuwa bora katika 'CRDB Bank Taifa Cup 2020 na 2021' (MVPs) uliochezwa jana kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay, jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment