Waziri wa Fedha na Mipango Dokta Mwigulu Nchemba akizungumza kwenye hafla hiyo. |
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi akizungumza kwenye hafla hiyo. |
Dodoma, 3 Juni, 2022 - Waziri wa Fedha na Mipango Dokta Mwigulu Nchemba amepokea gawio la shilingi bilioni 4.5 linalotokana na uwekezaji wa Serikali ndani ya Benki ya NBC. Serikali inamiliki asilimia 30 ya hisa za Benki hiyo.
Akizungumza katika hafla hiyo Dkt. Nchemba aliipongeza Benki ya NBC kwa kutoa gawio kwa Serikali na kuakisi mafanikio ya sera ya ubinafsishaji ya serikali iliyolenga kubinafsisha mashirika ya umma ili kuyaongezea tija na ufanisi.
“Serikali inajivunia mafanikio ya Benkl ya NBC kwani Benki hii ni moja ya mashirika ya kwanza kabisa kubinafisihwa nchini. Gawio hili la shilingi bilioni 4.5 mnalolitoa leo ni zaidi ya mara tatu ya gawio mlilotoa mara mwisho, hiki ni kiashiria tosha kwa Serikali kuwa Benki yetu ya NBCipo katika mstari sahihi”, alisema Dkt. Nchemba.
Waziri Nchemba pia alipongeza Benki ya NBC kwa matokeo mazuri ya fedha ambapo ilipata faida ya shilingi bilionin 60 ambalo ni ongezeko la asilimia 702 kwa matokeo ya mwaka 2020. Vilevile, Waziri Nchemba alipongeza jitihada za Benki ya NBC katika kuchangia maendeleo ya Taifa ikiwamo ulipaji wa kodi ambapo mwaka jana ililipa jumla ya shilingi bilioni 20 kama kodi.
“Napongeza sana mchango wenu katika uchumi wa taifa. Hakika nyinyi ni mfano wa kuigwa. Uwekezaji wenu katika jamii umekuwa chachu kubwa ya maendeleo. Napongeza sana sera yenu katika msaada kwa jamii ikiwemo uwekezaji katika ligi ya soka ya mpira ya NBC Premier league na uandaaji wa mbio za NBC Dodoma Marathon ambazo zinalenga kukusanya fedha za kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya kizazi kwa wanawake” alisema Dkt.Nchemba.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi aliishukuru serikali, kwa kuendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji na ufanyaji biashara nchini ambazo zimepelekea Benki kufanya vyema sokoni.
”Faida hii ambayo Benki ya NBC imepata na kuwezesha ulipaji huu wa gawaio la serikali, ina akisi mazingira bora ya biashara nchini. Tunajivunia pia kuweza kulipa kodi ya zaidi ya shilingi bilioni 20 kwa mwaka 2021 na kusaidia kupatikana ajira nyingi kupitia uwekezaji wetu katika ligi ya mpira nchini ya NBC Premier league.
Akizungumzia kuhusu mchango wa Benki kwenye ustawi wa jamii, Sabi alisema” kupitia sera yetu ya msaada kwa jami, tunajivunia kuwekeza katika kutatua changamoto nyingi za jamii ikiwemo uandaaji wa mbio za NBC Dodoma Marathon zenye lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya saratani ya shingo za kizazi kwa wanawake” alisema.
No comments:
Post a Comment