Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 10 May 2022

SHIRIKA LA FEDHA DUNIANI (IMF) LATUMA TIMU KUTATHIMINI HALI YA UCHUMI NCHINI

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akimkaribisha Mshauri wa Uchumi na Fedha kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) – Idara ya Afrika, Bw. Charambos Tsangarides, anayeongoza Timu ya Wataalam kutoka Shirika hilo kwa ajili ya kufanya tathimini ya hali ya uchumi na kisera, ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa mpango wa Shirika hilo wa kuipatia Tanzania mikopo na Misaada zaidi ya kutekeleza miradi ya maendeleo, Ofisini kwake Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza jambo na Mshauri wa Uchumi na Fedha kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) – Idara ya Afrika, Bw. Charambos Tsangarides, aliyepo nchini kwa ajili ya kufanya tathimini ya hali ya uchumi na kisera, ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa mpango wa Shirika hilo wa kuipatia Tanzania mikopo na misaada zaidi ya kutekeleza miradi ya maendeleo, Ofisini kwake Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati), akizungumza wakati wa kikao cha tathimi ya kazi inayoendelea kufanywa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) hapa nchini kuhusu hali ya uchumi na kisera, Jijini Dodoma. Kushoto ni Kiongozi wa Timu hiyo ambaye ni Mshauri wa masuala ya Uchumi na Fedha wa (IMF) – Idara ya Afrika, Bw. Charambos Tsangarides na kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel Tutuba.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa pili kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Wataalam kutoka Shirika la Maendeleo la Kimataifa (IMF) inayoongozwa na Mshauri wa Shirika hilo anayesimamia Idara ya Afrika, Bw. Charambos Tsangarides, Jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel Tutuba na kushoto ni Bw. Marcos Ribeiro kutoka IMF.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa sita kulia) ukiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Wataalamu kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), ikiongozwa na Mshauri wa Uchumi na Fedha wa Shirika hilo Bw. Charambos Tsangarides (wa nne kushoto), Ofisini kwa Waziri wa Fedha na Mipango Jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment