Maafisa wa NMB katika picha ya pamoja wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya Ubunifu Kitaifa, iliyofanyika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. |
Cheti hicho kilikabidhiwa wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Ubunifu Kitaifa yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma jana na kupokelewa na Mkuu wa Idara ya Ubunifu wa Benki ya NMB – Josina Njambi pamoja na Mkuu wa Idara ya Huduma za Serikali na Ofisi ndogo za Makao Makuu Dodoma – Vicky Bishubo.
Aidha, kabla ya kukabidhi cheti hicho, Makamu wa Rais, Mhe Dkt. Mpango alitembelea banda la NMB ambapo Josina alimueleza kuhusu fursa ambayo benki ya NMB imewaletea wabunifu kupitia mfumo wa NMB Sandbox Environment.
“Tumekuja na mfumo huu wa majaribio kwa ajili ya Vijana wabunifu wenye suluhishi za kifedha kujaribu masuluhisho yao kisha kuwasaidia wabunifu hao kuingia sokoni,” alisema Josina.
“Mpaka sasa wapo wabunifu zaidi ya 150 ambao wanaendelea kufanya majaribio ya suluhishi zao katika mfumo huu.”
No comments:
Post a Comment