Meneja wa Dun & Bradstreet Tanzania, Junaid Malik. |
Dun & Bradstreet Credit Bureau Tanzania ni taasisi inayoongoza kwa kukusanya na kuchakata taarifa zinazomtambulisha mtu binafsi au kampuni/taasisi kwenda kwa taasisi zinazotoa mikopo kwa watu binafsi, mashirika pamoja na taasisi za kifedha kutoka vyanzo mbali mbali na kusizambaza taarifa hizo kwa wateja wake. Taarifa hizi (Data) husambazwa katika mfumo wa Ripoti ya Taarifa ya Mikopo na utumika katika kuwezesha wakopeshaji kutathmini ustahili, tabia na historia ya ulipaji wa madeni kwa mkopaji.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza kupatikana Ripoti za Taarifa ya Mikopo (CIRs) pamoja na maelezo kwa watumiaji wake kwa lugha ya Kiswahili, Meneja wa Dun & Bradstreet Tanzania, Junaid Malik alisema, ‘Kwa leo ni hatua kubwa na muhimu kwetu kwa kuweza kutoa ripoti hizi kwa lugha ya Kiswahili. Hii inathibitisha dhamira yetu ya kuendelea kuwahudumia wateja wetu kwa huduma bora zaidi. Hatua hii itafanya ripoti hizi kueleweka vizuri na zaidi na zitawafanya wakopeshaji pamoja na wakopaji kuzitumia kwa ubora zaidi’.
Malik aliongeza kuwa lugha ya Kiswahili ndio lugha mama kwa Watanzania. Kupatika kwa ripoti pamoja na taarifa hizi kwa lugha hiyo zitaongeza uelewa zaidi na kuwafanya wakopaji kusimamia mikopo yao na kuwa na nidhamu nzuri ya ukopaji wa fedha.
Malik alisema, ‘Wakati Ripoti zetu za Taarifa ya Mikopo zikiendelea kuwa kuwa rahisi kwa kuelewa na upatikanaji wake, bado zinaendelea kubaki kuwa muhimu sana kwenye kufanya maamuzi. Taarifa na ripoti hizi zinajumuisha maelezo ya mkopaji pamoja na alama za kulipa mkopo, viashiria vya uwezekano wa kulipa mkopo pamoja na taarifa za mikopo inayopatikana kutoka makampuni ya mitandao ya simu za mkononi. Taarifa hizi pia hutoa maelezo ya mkopo wa mtu binafsi na uwezekano wa kurejesha hata pale hali inapokuwa tofauti na matarajio. Vile vile, taarifa ya mikopo ina alama ya mkopo iliyotengenezwa kwa ubashiri na kwa kuzingatia hali na mazingira ya mfumo wa fedha wa Tanzania.
Dun & Bradstreet Credit Bureau Tanzania inasimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania chini ya kanuni za 2012 (CREDIT REFERENCE BUREAU)
No comments:
Post a Comment