Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 22 February 2022

MAENDELEO KATIKA SEKTA YA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI

Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Jacqueline Woiso.
  • Mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan
Nukuu za Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Jacqueline Woiso katika mjadala wa Maendeleo katika sekta ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari uliofanyika hivi karibuni.

“Mimi kama Mdau katika sekta ya Habari ninaweza kusema kuwa tumeona maendeleo katika sekta ya visimbuzi, hususan katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan. Ndani ya mwaka mmoja kuna mabadiliko makubwa yametokea na yanajenga msingi wa ukuaji endelevu wa sekta ya visimbuzi hapa nchini.

Ushirikishwaji wa wadau; Katika kipindi cha uongozi wa Mama Samia, tumeshuhudia kuimarika sana kwa ushirikishwaji wa wadau katika kujadili na kufikia maamuzi ya masuala yanayohusu sekta ya visimbuzi hapa nchini pamoja na Wadau wengine wakiwemo vituo vya Utangazaji na wazalishaji wa Maudhui ya mtandao (online content providers).

Marekebisho ya kanuni za utangazaji; Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, umefanyika mchakato wa mabadiliko ya kanuni za sekta ya Habari ikiwemo ya utangazaji. Mchakato huo ulikuwa shirikishi na hatimaye tarehe 31 January mwaka huu, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye aliidhinisha marekebisho ya kanuni za sekta ya utangazaji ambapo kwa upande wa visimbuzi, iliruhusu kuonekana kwa chaneli za ndani (Local Channels) kupitia mfumo wa satellite.

Kupanua wigo wa local content; Chaneli za DStv zinaonekana katika nchi zaidi ya 36 barani Afrika hivyo walaji wa maudhui wanakuwa wengi siyo tu ndani ya nchi bali hata nje ya mipaka ya nchi yetu. Kufuatia mabadiliko hayo, tutaweza kutangaza bidhaa na huduma zinazozalishwa Tanzania na kuongeza biashara ya matangazo sio tu kwenye content.

Kuchochea ubunifu katika sekta ya Sanaa, Utamaduni na Michezo; Wasanii wengi wamefaidika kwa kuonekana ndani na nje ya nchi. HUBA mwaliko Dubai na Tamthilia ya Jua Kali imepata tuzo zaidi ya 10 ikiwemo ya TZ Film Awards Tamthilia bora mwaka jana. Uwekezaji unaongezeka mwaka hadi mwaka.

Kudhibiti Uharamia; Tumeona juhudi kubwa kati ya Wizara ya Habari na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kudhibiti uharamia (content piracy) ambayo imekuwa ni changamoto kubwa katika kukuza biashara ya visimbuzi nchini. Uharamia unasababisha upotevu wa kodi na kuvunja sheria za hakimiliki za wasanii wetu wa kitanzania.

Mapato kwa Serikali; marekebisho haya yanatoa fursa kwa biashara ya visimbuzi kuongezeka na kuchangia zaidi katika pato la Taifa kupitia kodi mbali mbali zinazolipwa na makampuni husika, wafanyakazi, mawakala, Content producers, Wasanii, makampuni ya simu n.k.”

No comments:

Post a Comment