Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 22 February 2022

BENKI YA CRDB YAWAPA SOMO LA FEDHA WAMACHINGA DAR

Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi, Stephen Adili akizungumza wakati wa ufunguzi wa Semina ya Elimu ya Fedha kwa Wamachinga iliyoendeshwa na Benki ya CRDB tarehe 20/02/2022 katika ukumbi wa PTA Sabasaba. Mafunzo haya yamehudhuriwa na Shirikisho la Umoja wa Wamachinga mkoa wa Dar es salaam (Machinga Saccos) na baadhi ya wawakilishi wa wafanyabiashara hao kutoka Mikoa yote Tanzania ikiwa ni mwendelezo wa ushirikiano tulionao kati ya Benki yetu na wafanyabiashara wadogo (Wamachinga).
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Mashariki, Badru Idd akizungumza wakati wa ufunguzi wa Semina ya Elimu ya Fedha kwa Shirikisho la Umoja wa Wamachinga mkoa wa Dar es salaam lililoendeshwa na Benki ya CRDB tarehe 20/02/2022 katika ukumbi wa PTA Sabasaba, Dar es salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Umoja wa Wamachinga mkoa wa Dar es salaam, Steven Lusinde akizungumza wakati wa ufunguzi wa Semina ya Elimu ya Fedha kwa Shirikisho la Wamachinga mkoa wa Dar es salaam lililoendeshwa na Benki ya CRDB tarehe 20/02/2022 katika ukumbi wa PTA Sabasaba, Dar es salaam.






















No comments:

Post a Comment