Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan hivi karibuni aliwaalika Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika Sherehe za Mwaka Mpya 2022 kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) Ikulu – Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, katika sherehe hizo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alisema Sera Mpya ya Mambo ya Nje itaendelea kuzingatia Diplomasia ya Uchumi na kuakisi maendeleo mapya kama vile uchumi wa bluu, mabadiliko ya tabianchi, uchumi wa kidigitali pamoja kukuza lugha ya Kiswahili kama lugha ya kidiplomasiana kibiashara.
Awali, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula aliwahakikishia Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na Waakilishi wa Mashirika ya Kimataifa kuwa Tanzania chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuimarisha uhusiano wake kila wakati.
No comments:
Post a Comment