Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala akizungumza jambo katika hafla hiyo. |
- Azindua Wiki ya Huduma kwa wateja China Dasheng Bank.
RC Makalla pia ametoa wito kwa Taasisi hizo kubuni bidhaa zinazoendana na wakati husika ikiwa ni pamoja na mikopo yenye riba nafuu.
Aidha RC Makalla ameipongeza Benki ya China Dasheng iliyoanzishwa miaka miwili iliyopita kwa kutengeneza faida ya Shilingi bilioni 5 na kuwa na mtaji wa bilioni 112.
Hata hivyo RC Makalla ametoa wito kwa benki hiyo kutanua huduma za matawi mikoani na nchini China ili kuwasaidia Wafanyabiashara wanaoendesha Biashara nchini China.
Pamoja na hayo RC Makalla amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya biashara ili kuvutia Uwekezaji na amewahakikishia usalama.
No comments:
Post a Comment