Kampeni hiyo inalenga kuwafanya wateja wa Serengeti Lite kufurahia ladha ya kipekee ya bia hiyo ya Kitanzania, iliyotengenezwa Tanzania kwa ajili ya Watanzania huku wakionyesha vipaji na uwezo wao.
Kwa mujibu wa meneja mwandamizi wa chapa wa Serengeti Wankyo Marando, kampeni hiyo ni maalum kwa watu na vijana wenye uthubutu, wanaojiongeza na ambao pia wanaofanya zaidi na zaidi ili kufikia malengo waliyojiwekea bila woga wala kuangalia nyuma.
Kampeni hiyo itakayodumu kwa miezi mitatu, itahusisha mashindano ya kuwapata JD wakali na jumla ya washiriki 5,200 kutoka shehemu mbali mbali nchini watapewa jukwaa la kuonyesha vipaji vyao. Washindi watatu watapata zawadi ya DJs kits zenye thamani ya hadi shilingi milioni saba kila moja huku wakipewa nafasi za kufanya kazi kama ma DJ wa Serengeti Lite katika sehemu wanazoishi.
Washiriki ambao hawataweza kufika fainali, watapata zawadi mbali mbali kama baketi za bia, tisheti, kofia Pamoja na kupata jukwaa la kuonyesha vipaji vyao chini ya chapa ya bia inayoheshimika na kupendwa, Serengeti Lite.
Kwa mujibu wa Wankyo, shindano ka kuwapata ma DJs wakali wanaochipukia lipo wazi kwa mtu yeyote mwenye umri wa miaka zaidi ya 18 na ambaye anaamini kuwa ana kipaji.
“Mtu yeyote mwenye umri zaidi ya miaka 18 anaweza kushiriki kwenye shindano hili katika sehemu alipo kwa kuwa linafanyika nchi nzima. Matanganzo ya wapi linafanyika yatakuwa yakitolewa katika kila wilaya na mkoa kupitia magari ya matangazo, redio Pamoja na kurasa za mitandao ya kijamii za Serengeti Lite.
Ili kushiriki, washiriki watatakiwa kujiandikisha katika baa zitakazotangazwa na ambazo mashindano hayo yatafanyika na pia watatakiwa kuwa na orodha ya nyimbo watakazozicheza. Kutakuwa na mashindano kila wiki na mashindanao yatafanyika katika ngazi ya wilaya, mkoa na kitaifa ambapo washindi watatu watapatikana.
Wankyo alisema washindi watapatikana kwa kupigiwa kura ambapo majaji watakuwa na asilimia 60 ya kura zote na asilimia 40 itakuwa ni ya mashabiki. Mashabiki wanaweza kushiriki kwa kupihga kura moja kwa moja wakiwa eneo la tukio au kupitia kurasa za mitandao ya kijamii za bia ya Serengeti Lite.
Meneja huyo wa chapa aliwataka vijana kuchangamkia fursa hiyo itakayowapa nafasi ya kupiga hatua katika kile wanachokipenda.
No comments:
Post a Comment