Benki ya Biashara ya DCB imesema itaendelea kuboresha na kuingiza sokoni bidhaa na huduma mbalimbali za kidigitali kwa lengo la kusogeza huduma zake karibu kwa wateja ikiwa ni pamoja na kuhakikisha watanzania wanapata huduma za kibenki kwa haraka na kwa gharama nafuu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Biashara wa DCB, Zacharia Kapama alisema uboreshaji huu wa huduma zetu za kibenki kwa njia ya kidigitali unaonyesha nia yetu ya kufanya benki yetu kuzidi kupiga hatua na kuwa chaguo namba moja kwa kila anaehitaji huduma za kifedha nchini kwa haraka na gharama nafuu.
“Uboreshaji wa huduma za kibenki kwa njia ya kidigitali ni moja ya tukio lingine la kihistoria la Benki ya DCB katika kudhihirisha kwa dhati nia yetu ya kufanya mabadiliko katika benki yetu kuzidi kupiga mwendo na kuwa chaguo namba moja kwa kila anayehitaji huduma za kifedha nchini kwa haraka na gharama nafuu.
“Uboreshaji wa huduma za kibenki kidigitali ni moja ya mikakati ya DCB katika kuhakikisha benki yetu inakwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na kiteknolojia yanayoendelea duniani kote katika kubuni mbinu rahisi na za haraka za kufikisha huduma za kibenki karibu na mteja”, alisema Bwana Kapama.
Alisema DCB kwa kitambo sasa imeendelea kutoa huduma mbalimbali kwa njia ya mtandao, kama mnakumbuka mwaka 2018 tulizindua huduma za DCB Pesa na hadi leo wameweza kusajili wateja zaidi ya 200,000 wanaotumia huduma zao za kidigitali. Huduma hizi zilipokelewa kwa muamko mkubwa na hadi leo wateja wa DCB wanaweza kukopa na kufanya marejesho kwa njia ya kidigitali.
Alisema Kutokana na mabadiliko ya chapa ya benki yao waliyokamilisha miezi michache iliyopita,benki sasa imeendelea kuja na njia mbalimbali za kutoa huduma kidigitali huku wakitambua kuwa dunia ya sasa imekuwa dunia ya kidigitali huku kila tasnia ikiongeza ubunifu katika kubuni teknolojia zikazofanya suala la utoaji huduma mbalimbali lifanyike kwa haraka, rahisi, ubora na unafuu.
Huduma za kibenki kwa njia ya kidigitali zimesaidia sana katika kuhakikisha wateja wengi wanafikiwa na huduma za kibenki kwa urahisi, ukaribu na kwa gharama nafuu hivyo kuwa mkombozi kwa watanzania wengi waishio mahali ambapo hakuna mtandao wa matawi yabenki.
Huduma pendwa zifuatazo ni rafiki na gharama nafuu hivyo tunawakaribisha kwenye mwendo huu wa kidigitali.
Akizungumzia zaidi alisema sasa wananchi wote wanaweza kulipa kodi na ushuru kupitia mfumo mpya wa malipo ya serikali (GePg) katika matawi yetu yote na kupitia huduma za kimtandao na kwa njia ya simu. Malipo ya serikali ni pamoja na Malipo ya manispaa zote za Dar es salaam, Mamlaka ya bandari (TPA), Mamlaka ya mapato (TRA), shirika la bina (NIC) na Mamlaka ya anga, Hospitali ya Muhimbili na kadhalika.
Vilevile aliongeza kuwa mteja anaweza kufanya malipo ya taasisi mbalimbali moja kwa moja kwa kutumia akaunti yako ya DCB kwenda kwenye taasisi, maduka na biashara zaidi ya 50,000 Tanzania nzima kwa kupitia huduma ya lipa namba ya selcom Mastercard QR.
Aidha akizungumza kuhusu mfumo wa mawakala wa DCB mkurugenzi huyo alisema benki imeboresha mtandao imara wa mawakala kwa kuanzisha mawakala wakubwa (Super Wakala) unaohudumia wateja bila uhitaji wa kufika katika matawi nchi nzima. Vilevile benki imesogeza huduma za kibenki kwenye manispaa zote za dar es salaam na mikoani lengo kuwarahisishia wananchi kufanya miamala kwa haraka na nafuu.
Kuhusu huduma zake kwa njia ya simu za mkononi Bwana Kapama alisema hii ni huduma maalum inamuwezesha mteja kufungua akaunti ya DCB Pesa kwakupiga *150*85# kwa wenye simu za kawaida ama wale wenye simu janja kwa kupakua APP ya DCB Pesa kwenye playstore kwa njia ya simu ya mkononi na kufanya miamala popote alipo kwa gharama nafuu.
Alisema akaunti hii pia inamuwezesha mteja kuweka akiba kidogo kidogo kwa ajili ya kufanikisha kwa malengo yake huku akipata riba hadi asilimia 10 kwa mwaka na pia mkopo wa hadi asilimia 80 ya kiasi alichojiwekea yote haya yakifanyika kwa kupitia simu ya mkononi.
“Vilevile akaunti inakupa fursa ya kuweke za kupitia Digital FDR ambayo inakupa riba ya kiushindani. Digital lamba kwanza inayokuwezesha kupata riba papohapo unapowekeza. lakini pia kupitia DCB pesa unapata huduma kama Digital Salary advance, Mkopo wa dharura, malipo ya dawasco,luku,ving’amuzi. Huduma hizi za Kidigitali zinazotolewa na Benki ya DCB zimepokelewa kwa muitikio mzuri na wateja wetu. DCB tutaendelea kutoa huduma bora na kuhakikisha tunawapatia wateja wetu bidhaa bora zinazoenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na kiteknolojia na mahitaji ya soko kukidhi ndoto za wateja wetu.
“Benki ya DCB imeendelea kutoa uhuru wakufanya miamala kwa wateja wake kwa kuwawezesha wateja kutumia kadi za visa. Mteja sasa anaweza kufanya miamala popote duniani kwa kutumia DCB Visa Cards.
“Benki ya DCB ambayo hivi karibuni ilibadilisha chapa na muonekano wake kutoka ule wa zamani, imeendelea kukua na kupata faida mwaka hadi mwaka nakupiga hatua kubwa za kimaendeleo ikiwa na muonekano mpya wa benki kamili ya Kibiashara haya yakiwa ni matunda ya ushirikiano madhubuti kutoka menejimenti yetu pamoja na wafanyakazi wetu makini.
”Tunatoa wito kwa wateja wetu wote na watanzania kuchangamkia fursa zipatikanazo na benki yetu. Kwani kupitia mtandao wetu wa huduma za kidigitali unaweza kupata huduma mbalimbali bila gharama yoyote kama kuangalia salio bure, kuhamisha fedha kwenda akaunti nyingine bure, kutuma au kupokea pesa kwenda mitandao mingine bure, kutoa pesa kwa mawakala bure, kuweka pesa kwa mawakala bure, kutoa pesa kwenye ATM bila kadi na huduma nyinginezo”,aliongeza Bwana Kapama.
No comments:
Post a Comment