Kitomari Banking & Finance Blog is a premier site for banking, finance, business, economic, investment and stock market news as well as selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the World. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.
Thursday, 29 July 2021
Wednesday, 28 July 2021
WASANII WA ZANZIBAR WANOLEWA
EQUITY BANK (T) INTRODUCES INTERBANK MONEY TRANSFERS AND SADC (SIRESS) SERVICES TO BOOST CROSS BOARDERS' AND REGIONAL REMITTANCE SERVICES.
- Customers with Equity Bank accounts can now transact seamlessly in any of the Equity Bank branches across Africa.
- SIRESS services to boast and facilitate monetary transactions to and from the SADC block at the cost of USD 10 only regardless of the amount
Speaking at an event in Dar es Salaam yesterday, Equity Bank Managing Director Robert Kiboti said: "We are proud to provide a reliable financial link between Equity Bank Tanzanians customers with the rest of Equity bank network through our One Equity Inter-Country services that allow seamless real-time transactions at a minimal cost. Simply, Equity Bank Customers will be able to make deposits, receive deposits, and make withdrawals at any Equity Bank branch online in Kenya, Uganda, Rwanda, South Sudan, and Congo DRC as a domicile country. Also, Equity customers can now transfer to an Equity customer in any country of operation. Through our world-class digitization of the product, Equity Bank customers will enjoy the freedom of accessing all these services at their convenience of Eazzy Banking App-, and Eazzy Net& Eazzy Biz- Intercountry Funds transfer on our online banking platforms.
"The primary purpose of the product is to provide solutions for Equity customers and non-customers (deposit only) across the Group to access their accounts and transact from any of the Equity Bank group subsidiaries, in any of the local currencies. "We believe this will be an important solution to facilitate cross-border payments between Tanzania, Kenya, Congo DRC, Rwanda, and the rest of Equity network. I call upon all cross-border traders, including SMEs, Transporters, and the likes to capitalize on these new services from Equity Bank," said Mr. Kiboti.
NMB YAKABIDHI HUNDI YA SH. MILIONI 438.4 KWA WAHANGA WA MOTO KARIAKOO
Hafla ya kuwakabidhi wafanyabiashara hao hundi hiyo, imefanyika katika Tawi la NMB Kariakoo Business Center, ambako wahanga hao walikiri kuwa hasara na maumivu yao ya kuunguliwa yamepozwa na malipo hayo ya haraka ya bima.
Akizungumza kabla ya kuwakabidhi hundi ya mfano, Mkuu wa Kitengo cha Bima Benki ya NMB, Martine Massawe, alitoa wito kwa Watanzania kujenga utamaduni chanya wa kuzilinda kwa bima mali na pesa wanazotafuta kwa jasho, ili kuepuka maumivu yasiyo na mfariji wakati wa majanga.
“Tuko hapa kwa ajili ya kuwafuta machozi wafanyabiashara waliokata bima nasi kupitia mikopo yao ama waliokuwa na bima za mali bila mikopo, ambao walikuwa sehemu ya wahanga wa moto sokoni Kariakoo.
“Wito kwa Watanzania, moto wa Soko la Kariakoo uwe fundisho kwao juu ya umuhimu wa bima. Moto ama majanga huja bila kuyatarajia, unapokata bima unakuwa umejiwekea kinga kuilinda pesa ama mali uliyotafuta kwa jasho lako.
Tuesday, 27 July 2021
AMANA BANK YAZINDUA PROGRAMU YA KIDIGITALI INAYOWEZESHA HUDUMA ZA KIISLAMU
Wafanyakazi wa Benki ya Amana wakijaribu matumuzi ya App hiyo wakati wa uzinduzi uliofanyika Dar es Salaam. |
Wateja wa Amana Bank wakipatiwa maelezo ya matumizi ya teknolojia hii mpya ya kidigitali wakati wa hafla ya uzindzi. |
Amana Bank Limited, inayoongoza kwa kutoa huduma za Kibenki za Kiisilamu nchini Tanzania, leo imetangaza kuwa imefanya mapinduzi ya huduma zake za kibenki kupitia simu za mkononi kwa kuanzisha programu mpya kupitia simu za mkononi, inayomwezesha mteja kufanya malipo na huduma za kibenki kwa wateja wake iitwayo Amana Bank App; Programu inawezesha kupata huduma za kibenki kidigitali kama vile kufanya malipo, kuhamisha fedha, kulipa bili na kufanya malipo mtandaoni, kupokea taarifa za benki na kupokea habari juu ya huduma zinazotolewa na benki kama mikopo, viwango vya ubadilishaji wa kigeni na hata kulipia huduma mbalimbali kama malipo ya serikali na huduma za bima.
DC NYAMAGANA: WANAWAKE CHANGAMKIENI FURSA ZINAZOLETWA NA NMB
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa NMB, Alex Mgeni akipokea bidhaa zilizosindikwa na Mjasiriamali, Doroth Kimati anayewezeshwa na NMB katika uzinduzi wa Klabu ya "NMB Mwanamke Jasiri" jijini Mwanza. Katikati ni Mjasiriamali, Hellen Bugoye. |
Baadhi ya akina mama wajasiriamali wakifuatilia hotuba mbalimbali kwenye uzinduzi wa Klabu ya "NMB Mwanamke Jasiri" jijini Mwanza. |
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi, akizungumza wakati akizindua Klabu ya "NMB Mwanamke Jasiri" jijini Mwanza. |
Mkuu huyo wa wilaya aliyasema hayo alipokuwa anazungumza na umati wa wanawake na wakazi wengine wa mkoa huo waliohudhuria uzinduzi wa klabu ya ‘mwanamke jasiri’ mkoani Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla.
Bi. Makilagi alisema kuwa wakazi wa Mwanza wasiache kuchangamikia fursa zinazoletwa na benki ya NMB kwani benki hiyo ina malengo mazuri ya kutaka kuleta maendeleo kwa wateja wake.
Monday, 26 July 2021
DStv INAKULETEA CHANELI MPYA YA BURUDANI
DStv wakali wa burudani wanakuletea Chaneli mpya itakayokuwa ikirusha filamu kali za Afrika Mashariki (Tanzania, Kenya na Uganda).
Pata kuburudika na filamu hizi kupitia Chaneli ya Maisha Magic Movies 141, itakayoanza kuruka kuanzia leo tarehe 26 July 2021, saa 10 jioni.
Kulipia kifurushi chako piga *150*53# ili usikose burudani hii.
Pata kuburudika na filamu hizi kupitia Chaneli ya Maisha Magic Movies 141, itakayoanza kuruka kuanzia leo tarehe 26 July 2021, saa 10 jioni.
Kulipia kifurushi chako piga *150*53# ili usikose burudani hii.
BENKI YA NMB KUWAKOPESHA WACHIMBAJI MADINI WADOGO ZAIDI YA SH. 120 BILIONI
Sehemu ya wageni waalikwa ambao ni miongoni mwa Wachimba Madini wa Kanda ya Ziwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa 'NMB Mining Club' uliofanyika katika Hoteli ya Gold Crest - Mwanza. |
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi, Robert Gabriel Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa ‘NMB Mining Club’ kwa Kanda ya Ziwa. |
“Wachimbaji wadogo watakopeshwa vifaa na mitambo bila kulazimika kuweka dhamana kwa sababu mitambo na vifaa hivyo ndivyo vutakuwa dhamana yao baada ya kulipa kuanzia asilimia 20 ya thamani ya kifaa au mtambo anaotaka kununua,” alisema Mgeni.
Akizuzugumza wakati wa hafla hiyo iliyoshirikisha wachimbaji zaidi ya 200 kutoka mikoa ya Mwanza, Mara, Simiyu, Geita, Shinyanga na Kagera, Rais wa Shirikisho la Wachimba Madini Tanzania (Femata), John Bina alisema uamuzi wa benki ya NMB kuanzisha dirisha la mikopo kwa Sekta ya Madini siyo tu utaongeza tija, bali pia utakuza uchumi wa wachimbaji na Taifa kwa ujumla.
Friday, 23 July 2021
WAKUU WA MIKOA YA SINGIDA NA MOROGORO WAKIRI NMB KUWA CHACHU YA KUKUZA UCHUMI WA WAALIMU
Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Mwembesongo, Abdula Omary akichangia mada wakati wa kongomano la Benki ya NMB na Walimu lililofanyika Mkoani Morogoro. |
Wakuu wa Mikoa ya Singida na Morogoro, Dr. Binilith Mahenge na Martin Shigela kwa nyakati tofauti wamekiri kuwa benki ya NMB imekuwa kinara katika kuimarisha waalimu kiuchumi kupitia huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo.
Wakizungumza katika warsha za siku ya mwalimu ambazo huandaliwa na Benki ya NMB katika mikoa yao, Wakuu hao wamewasisitiza Waalimu kuzitumia vyema huduma za benki hiyo katika kujiimarisha kiuchumi.
Katika warsha ya mkoani Singida, Mkuu wa Mkoa huo, Dr. Mahenge alisema kuwa NMB imekuwa na huduma nzuri zaidi za mikopo ambayo ni rafiki na haina masharti magumu kwa walimu. Hivyo akawasihi waalimu wachangamkie fursa hiyo na akashauri waweze kutumia mikopo hiyo katika kilimo cha alizeti ambayo inastawi sana mkoani hapo huku zao hilo likiwa chanzo kikubwa cha mapato katika mkoa wa Singida.
NMB YAKABIDHI MADAWATI YA SH. MILIONI 10/- MKURANGA
Benki ya NMB imetoa msaada wa viti 50, meza 50 kwa shule ya Sekondari ya Mkugilo na madawati 62 kwa Shule ya Msingi Chatembo, wilayani Mkuranga, Pwani vyote vikiwa na thamani ya Sh. Milioni 10.
Msaada huo, ulitolewa katika hafla iliyofanyika viwanja vya Shule ya Sekondari Mkugilo na Meneja Mahusiano, Biashara za Serikali wa NMB Kanda ya Mashabiki, Aneth Kwayu kwa niaba ya NMB na kumkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Khadija Nasser Ally.
Akizungumza katika hafla hiyo Aneth alisema kuwa NMB inazitazama changamoto za Sekta ya Elimu kama moja ya vipaumbele vyake vikuu, kutokana na ukweli kuwa elimu ndio ufunguo wa maendeleo sio tu ya mtu mmoja mmoja, bali pia kwa Taifa kwa ujumla- hivyo walivyopata maombi kuzisaidia shule hizi mbili waliona uhitaji na wamezisaidia.
Msaada huo, ulitolewa katika hafla iliyofanyika viwanja vya Shule ya Sekondari Mkugilo na Meneja Mahusiano, Biashara za Serikali wa NMB Kanda ya Mashabiki, Aneth Kwayu kwa niaba ya NMB na kumkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Khadija Nasser Ally.
Akizungumza katika hafla hiyo Aneth alisema kuwa NMB inazitazama changamoto za Sekta ya Elimu kama moja ya vipaumbele vyake vikuu, kutokana na ukweli kuwa elimu ndio ufunguo wa maendeleo sio tu ya mtu mmoja mmoja, bali pia kwa Taifa kwa ujumla- hivyo walivyopata maombi kuzisaidia shule hizi mbili waliona uhitaji na wamezisaidia.
DStv INAKULETEA CHANELI MPYA YA MAISHA MAGIC MOVIES
Kaa mkao wa kula sasa uweze kufurahia filamu za nyumbani na Afrika Mashariki ndani ya chaneli mpya ya #MaishaMagicMovies chaneli 141 inayokujia rasmi kuanzia tarehe 26 Julai 2021.
Hakikisha hupitwi na Utamu wa Chaneli hii kupitia kifurushi cha Compact TShs 49,000 tu kwa kupiga *150*53# kulipia kifurushi chako.
Wednesday, 21 July 2021
BENKI YA AZANIA YATOA BIMA KWA WAKULIMA ZAIDI YA 700 WA TUMBAKU
Mbeya. Julai 20, 2021 - Benki ya Azania kwa kushirikiana na mfuko wa bima ya afya (NHIF) pamoja na chama kikuu cha ushirika wa wakulima wa tumbaku wilaya ya Chunya, (CHUTCU) wamesaini makubaliano ya kuwawezesha wakulima wa zao hilo kujiunga na bima afya ili waweze kupata matibabu bure.
Makubaliano hayo yamefanyika Julai 19, 2021 kati ya Benki ya Azania Limited,NHIF na CHUTCU katika kata ya Lupatingatinga, halmashauri ya wilaya ya Chunya mkoani Mbeya na kushuhudiwa na mkuu wa wilaya hiyo Mayeka Simon Mayeka.
Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja Mwandamizi wa Biashara wa Azania Bank Limited, Jackson Lohay alisema katika makubaliano hayo benki hiyo itatoa mkopo usiokuwa na riba kwa ajili ya kuwawezesha wakulima zaidi ya 700 kupata bima ya afya.
“Katika mkataba wetu tutawawezesha wanachama ambao wapo chini ya chama kikuu cha ushirika ambao ni zaidi ya 700 lakini watakaonufaika na mpango ni zaidi ya watu 2000 wanaotegemewa na wanachama,’’ alisema
ZANTEL YAZINDUA KIJIJI CHA KIDIGITALI KUHAMASISHA MATUMIZI YA MTANDAO
- Watu kujifunza namna ya kujiendeleza kielimu na kuendesha biashara mtandaoni
Hatua hii ni miongoni mwa utekelezaji wa kampeni ya ‘Pasua Anga Ki Zantel 4G’ awamu ya pili, ambayo pamoja na mambo mengine ina lenga kutoa elimu kwa wakazi wa Zanzibar juu ya umuhimu wa mtandao wa 4G katika kuleta maendeleo ya kijamii na uchumi.
Mpango huo ni sehemu ya mkakati wa Zantel wa kuchochea mageuzi ya kimtandao na kufanya watu waishi kidigitali.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja Masoko wa Zantel-Zanzibar, Rukia Mtingwa alisema kuwa kituo hicho cha Kiditali kitatoa huduma za kimtandao bure kwa wakazi wa Zanzibar ndani ya miezi miwili.
BENKI YA DCB YAZIDI KUKUA NA KUPATA FAIDA; YAWAAMBIA WANAHISA WAKE KUTOKA HALMASHAURI YA JIJI LA ILALA
Baadhi ya madiwani, wakurugenzi na wakuu wa idara kutoka katika Halmashauri ya Jiji la Ilala wakihudhuria mkutano huo jijini Dar es Salaam. |
Baadhi ya madiwani, wakurugenzi na wakuu wa idara kutoka katika Halmashauri ya Jiji la Ilala wakihudhuria mkutano huo jijini Dar es Salaam. |
Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Saad Khimji (kulia), akizungumza katika mkutano huo. |
Tuesday, 20 July 2021
BAA ZAENDELEA KUCHANGAMKIA FURSA YA SBL ‘RAISE THE BAR’ AU 'TUNYANYUKE PAMOJA’
RAIS WA ZANZIBAR AVUTIA WASHIRIKI ‘NMB 5K RUN 2021’
Watoto nao pia walishiriki mbio za Kimataifa za Zanzibar Marathon za Kilomita tano zilizodhaminiwa na Benki ya NMB na kufanyika juzi visiwani Zanzibar. |
Watu mbali mbali walishiriki mbio za Kimataifa za Zanzibar Marathon za Kilomita tano zilizodhaminiwa na Benki ya NMB na kufanyika juzi viziwani Zanzibar. |
NMB 5K Run 2021 zilikuwa ni sehemu ya Zanzibar International Marathon - mbio zilizofanyika chini ya kaulimbiu ya 'Tunakuza Uchumi wa Bluu Kupitia Michezo Zanzibar, zilizoanzia Ngome Kongwe na kuishia Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, ambako Dk. Mwinyi alikuwa mmoja wa waliokimbia kilomita 5.
NMB ilidhamini kilomita 5 kwa Sh. Milioni 35, lengo likiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali ya Zanzibar katika kuhamasisha na kukuza utalii, kukuza Uchumi wa Bluu na kuchagiza jamii kudumisha utamaduni chanya wa kufanya mazoezi ili kuepukana na magonjwa yasiyoambukizwa.
Subscribe to:
Posts (Atom)