Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday, 4 June 2021

MECHI ZOTE ZA UEFA EURO 2020 NDANI YA DStv!


Pira Biriani kuanikiza Ulaya mwezi mzima!

Mchecheto wa washabiki washika kasi.

Wapenzi wa soka wa Tanzania sasa wameanza kuingia hamasa baada ya wakongwe wa burudani SuperSport kutangaza kwamba wataonyesha mubashara mechi zote za mashindano maarufu ya UEFA Euro 2020 kupitia kisimbuzi maarufu cha DStv.

Mkuu wa Masoko wa DStv Tanzania Ronald Shelukindo, ametangaza habari hizo njema kwa wanazi wa soka wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo DStv inauita msimu wa michuano hiyo kama msimu wa ‘Biriani Ulaya’. Katika kipindi hicho cha mwezi mmoja (Juni 11 – Julai 11, 2021), nyasi zitachimbika katikamadimba mbalimbali barani Ulaya ambapo timu za mataifa ya ulaya zitakabana koo kuwania ubingwa huo wa kifahari.

“DStv ni wababe wa burudani, na ukiongelea soka basi hapa ndiyo penyewe – hivyo watanzania wote wakae mkao wa kula, wasubiri kushuhudia Pira ‘Biriani Ulaya’ na mitifuano yote wataishuhudia mubashara kupitia DStv ndani ya chaneli zetu pendwa za SuperSport” amesema Shelukindo.

Kama kawaida yake na kwa fahari kubwa, ili kuongeza utamu na burudani kwa watanzania, DStv itatangaza michuano hiyo kwa lugha adhimu ya Kiswahili hivyo mtazamaji popote alipo kuanzia Nachingwea hadi Tarime, Mbinga hadi Kasulu, Pangani hadi Mpanda, wote wataweza kufuatilia michuano hiyo kwa lugha ya Kiswahili kupitia SuperSport ndani ya DStv.

“Sisi hatuwapimii wateja wetu burudani, tunataka uone kusikia na kuelewa kila kinachoendelea uwanjani. Hii ndiyo sababu tumeweka utaratibu wa kutangaza michuano hii kwa Kiswahili” alisema Shelukindo na kuongeza kuwa michuano hiyo itaonekana hadi kwenye vifurushi vya chini kikiwemo kile cha DStv Family na pia baadhi ya mechi zitaonyeshwa kwenye kifurushi cha chini kabisa cha DStv Bomba cha Sh. 19,900 tu!.

Pamoja na Michuano hii kufanyika mwaka huu 2021, bado itaitwa UEFA Euro 2020 ili kuadhimisha miaka 60 tangu michuano hii ya European Football Championship ilipoanzishwa mnamo mwaka 1920. Hii pia itasaidia kuunganisha wanamichezo wote kwa pamoja baada ya janga kubwa la Covid-19 na jinsi kila mmoja alivyoweza kupambana nalo kwa mwaka mzima wa 2020.

Michuano ya mwaka huu inajumuisha timu 24 zikiwemo timu zenye historia kubwa na zinazoogopewa katika soka duniani kama vile Ureno, Uingereza, Ufaransa, Hispania, Ujerumani, Italia, Ubelgiji na Uholanzi.

Mbali na kuwepo timu hizo kabambe, pia kuna wachezaji nyota ambao wanatarajiwa kuongeza ushindani katika michuano hiyo huku kila mmoja akitaka kuimarisha sifa na rekodi yake kimataifa. Nguli kama Christiano Ronaldo, Marcus Rashford, Burak Yilmaz, Romelu Lukaku na Kylian Mbappe wote wanatarajiwa kufanya yao katika michuano hii kitendo ambacho kinaongeza msisimko na bila shaka itakuwa patashika nguo kuchanika!

Michuano ya mwaka huu ambayo ni ya 16, ni ya kihistoria kwani kwa mara ya kwanza itatumia mfumo wa VAR (Video Assistant Referees). Ni michuano ambayo wababe wawili – Ujerumani na Hispania wanaingia huku wakiwa na historia ya kutwaa ubingwa mara tatu kila mmoja huku Ujerumani ikiwa ndiyo timu iliyowahi kucheza mechi nyingi zaidi (49) huku ikishinda mechi 26 na kufunga jumla ya mabao 72.

Kwa hakika hakuna mahali pengine utakapopata ladha ya michuano hii kama ndani ya Supersport. Watazamaji wa DStv wanauhakika wakushuhudia mechi zote za UEFA Euro 2020 kwa mwezi mzima kuanzia Juni 11 hadi Julai 11 2021 kwa kulipia kifurushi chako cha Family cha TZS 29,900/= tu kupitia chaneli ya Supersports

No comments:

Post a Comment