Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Monday 14 June 2021

BENKI YA AKIBA YASHIRIKI KATIKA ZOEZI LA KUTOA NA KUCHANGIA DAMU

Wafanyakazi wa Benki ya Akiba wakiwa kwenye maandalizi kabla ya kuanza zoezi la kuchangia damu lilofanyika jijini Dar es Salaam ikiwa ni maandalizi kuelekea maadhimisho yake June 14, 2021.
Baadhi ya wananchi wakiendelea na zoezi la kuchangia damu likiendelea jijini Dar es Saalam kuelekea kilele cha maadhimisho June 14, 2021.
Meneja Masoko wa Benki ya Akiba, Innocent Ishengoma akipima damu kabla ya kuanza zoezi la kuchangia damu lilofanyika jijini Dar es Salaam ikiwa ni maandalizi kuelekea maadhimisho yake June 14, 2021.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Akiba, Dora Siria (kushoto), akitambulishwa kwa mtaalamu wa kutoa damu na mchangiaji wa damu Masoud Kipanya wakati wa zoezi la kutoa na kuchangia damu iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Kama sehemu ya jamii pamoja na kutambua umuhimu w kuokoa maisha sisi kama taasisi tumeshiriki katika zoezi hili muhimu siku ya leo kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya kuchangia damu ambalo kilele cha maazimisho ni tarehe 14/06/2021.

Wafanyakazi kutoka Benki yetu wamejitolea kushiriki katika zoezi hili, kama nilivyosema kutokana na umuhimu wake pamoja na kuguswa mioyoni mwao kama wanajamii na sehemu ya jamii na pia kuunga mkono juhudi zake Benki katika kushiriki kwenye matukio ya kijamii. Benki ya Akiba imekuwa mshiriki mahiri katika maswala ya kijamii kwa kutoa misaada katika sekta za Elimu, Mazingira na Afya kama ambavyo siku ya leo tumeshiriki katika zoezi hili kuchangia damu.

Tunatoa rai kwa taasisi nyingine na Watanzania wote kwa ujumla kushiriki katika zoezi hili kwa ajili ya kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu wenye uhitaji wa damu.

No comments:

Post a Comment